TASISI YA UTAFITI WA MFUGO YAPATA HASARA MILINI 500 KUTOKA NA MGOGORO WA ARDHI KIBODYANI.



Na stephen noel  - Mpwapwa.
TASISI  ya utafiti wa mifugo  TALIRI  ilioko wilayani mpwapwa  mkoani Dodoma  imepata hasara ya  ya zaidi ya shilingi  milioni 500/= kutokana na  kuacha kuzalisha mifugo katika shamba lao la kibodyani  kutokana na mgogoro wa ardhi  kati ya tasisi hiyo na wanachi waishio katika kijiji hicho.
Mkurugenzi  wa tasisi hiyo  Dr. Daniel Komuhangilo  aliyasema hayo kituoani hapo alipokuwa akiongea na waandishi  wa habari  ofisi kwake  juu mgogoro wa a ardhi uliodumu  kwa muda wa miaka mmne sasa  tangu mwaka   2012.
Dr. Komuhangilo alisema  mgogoro huo kila siku zinavyo zidi  kusonga mbele ndipo  mgogoro huo unazidi kuchukua sura mpya na kuzidi kukomaa  na kuhatarishi hata uendelevu wa kituo hicho  kwa mstakabaili  wa Tanzania na nchi jirani  zinazo nufaika na kituo hicho .
Alisema mwaka 2012 kulitokea mgogoro  mipaka ya ardhi kati tasisi na wakazi wa kijiji cha kibodyani na kusababisha baadhi ya watumishi wa kituo walijeruhiwa na   mali za kituo hicho kuharibiwa ikiwemo gari.
  Na  alisema shitaka hilo lilifika katika mahakama ya wilaya ya Mpwapwa na baadhi watuhumiwa walipatikana na hatia  na walifugwa kifungo cha  miaka mitatu kifungo cha nje.
Alisema alishangazwa  na wanakijiji hicho  kuendelea kuingia kwenye maeneo  ya tasisi  hiyo ambayo ilikuwa  inatumiwa  kama shamba la kuzalishia ng’ombe wa utafiti ambao walikuwa wanazalishwa na kugawiwa  kwa  wakulima wa kanda ya kati na Tanzania  yote kutokana  ubora wa ngombe waliokuwa katika eneo hilo,
Aidha  aliongeza kuwa  kutokana na hali hiyo  tasisi hyo  imeshidwa kuzalisha ngombe hao kwa muda wa mika mine sasa  ambapo alisema  takribani ngombe 800 hawakuzalishwa  na tasisi hiyo kutokana na  mgogoro huo  ambao kwa sasa unazidi kushika kasi kila kukicha.
Aliongeza kuwa chanzo cha mgogoro huo ni  wakazi wa kijiji hicho kuingia kwenye mipaka ya tasisi hizo na kuanzisha  shughuli za kilimo   cha mahindi viazi na  mazao mengine kama maharage  na  njegere kinyume na utaraibu .
Alisema pia wananchi kutopenda kuheshimu maamuzi  ya kisheria  kutokana na kukingiwa  vifua na baadhi ya  viongozi hapa nchini kutapelekea   wanachi hao kuudharau mamlaka ziilizoko kwenye madarakani  na kutapelekea amani kutoweka katika maeneo  mengi hapa nchini.
Pia alisema  kuna baadhi wanasiasa  wanahusika kuchochea mgogoro huo  kwa maslahi yao binafsi ambayo ni kwa ajili ya kupata kura za uchaguzi  kwa mwaka huu 2015.
 Alisema  amepeleka barua ya tishio la amani katika kituo  hicho kwa mwenyekiti wa kamati  ya ulinzi na usalama  ambae ni mkuu wa wilaya ya mpwapwa  Christopher Kangoye  lakini alisema bado hajajabiwa kiofisi tangu wapelekee barua hiyo.
“Nimeongea nao mala kadhaa  kuhusu suala hilo lakini kila mala nimekuwa  nikijibiwa kuwa ebu niache kuwasumbua kwanza hasa katika mwaka huu wa uchaguzi”Aliongea  Dr. Komuhangilo
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mpwapwa  Christopher Kangoye alisema  hajapata taarifa za mgogoro huo kuendelea katika kijiji hicho  kutokana na usuluhishi ulio fanywa na  kamati ya ulinzi na uslama  ya wilaya hiyo.
Pia alisema kuwa mkurugenzi huo  awasilishe majina ya  wanasiasa wanachochoea mgogoro huo kituo cha polisi kwa hatua zaidi za kisheria “ maana hakuna mtu aliye juu ya sheria  juu ya sheria  hatuwezi kuvunja sheria za nchi kwa maslahi ya watu wachache  hiyo Tanzania hii inaongozwa kisheria  hivyo kila avunjae sheria atachukuliwa hatua  tu”aliongea Kangoye.
Amewataka wananchi  kutii sheria  bila shuruti ili kuweza kudumisha amani katika maeneo ya kazi na sehemu za makazi.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.