MWENYEKITI AVULIWA MADARAKA KWA TUHUMA ZA KUCHAKACHUA PESA YA KIJIJI MRADI WA MAJI.



Na noel stephen  - Chipogolo mpwapwa

Wakazi wa kijiji cha chipogolo  wilayani mpwapwa mkoani Dodoma  wamemvua madaraka  mwenyekiti wao wa kijiji   Wilson Manemo  kwa  tuhuhuma   kununua  Mashine mbovu ya kuvuta maji   kijijini hapo.
.
Waamuzi huo ulichukuliwa  na wanakijiji hao kufutia mwenye kiti huo kukiuka  makabariano ya wanakijiji  juu ununuzi wa mashine ya desel ya kuvuta maji  kijijini hapo ambapo pamoja na wajumbe wengine wawili walinunua mashine mbovu ambayo haifanyi kazi  kwa gharama tsh 8.500,000/=milioni nane na laki tano fedha za kijiji cha chipogolo.

Akiongea na mwanachi kaimu mtendaji wa kijiji hicho   Yona Mganga  alikili wananchi hao kuvua madaraka c mwenyekiti wa kijiji hicho kwa madi ya kutumia vibaya fedha za kijiji chao.

Mganga alisema   kufuatia mkutano wa kijiji ulio kaa 17 april mwaka huu  waliamua “kutokana na  uhaba wa maji uliopo katika kjijiji hicho  na kuharibika   mashine ya awali kijiji kiliagiza fedha zilizoko benki ya kjijiji  zitolewe na zika nunue enjinin mpya  ili kuweza kupunguza kero ya maji kijijini hapo”.

AIDHA alidai kuwa  “lakini kilichotokea mkutano huo uliamua  wajumbe wawili akiwemo mwenyekiti wakanunue mashine nyingine mpya ya kuvuta maji  kwa gharama y ashilingi million 6,500.000/= matokeo yake wajumbe hao walileta  mashine ambayo imetumika na  yenye gharama ya tsh 8,500,000/=  na haivifanyikazi kabisa ni mbovu”alieleza mganga na kuongezea

Alidai kuwa alipo fika wakati wa makabithiano  wajumbe wa kamati ya kjiji waligoma kupokea mashine hiyo kwa madai  ya kuwa mashine hiyo ni mbovu na kuwataka wajumbe walioenda kuinunua  kuitolea maelezo  lakini walishudwa  kuitolea maelezo ndipo wanakijiji waliikataa kuipokea mashine hiyo
,
Mwandisi wa maji wilaya ya mpwapwa Omar Mazola alikiri kuwepo kwa tatitizo hilo katika  kijijiji cha chipogoro na aliahidi kulifanyia kazi tatizo hili ikiwemo kuchukua hatua za kisheria kwa wote walio husika kwa njia moja au nyingine pindi itakapo bainika kuwa  mashine hiyo imechakachuliwa.

Alisema kuwa mashine iliyo nunuliwa ni  TR1 Desel Engine ambapo  amwewasilana na watu wa  TAMESA  kuja kudhibitisha mashine hiyo kuwa ni mpya au imetumika  ili kuweza kuondoa utata huo.

 Mpaka sasa kijiji hicho bado kina kabiliwa na adha kubwa ya ukosefu wa maji  kutokana na pamp ile iliyo kuwepo kharibaka  hivyo wananchi wa kijiji hicho hutumia maji ya kwenye madibwi amabayo si salama kwa afya za binadamu.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.