TAFITI ZITUMIKE KUONDOA CHANGAMOTO KATIKA JAMII. DC kizigo Mpwapwa.

  Na Mwandishi wetu.Mpwapwa.


Serikali imeobwa  kuzitumia tafiti mbalimbali zinazofanywa na tasisi mbaliimbali hapa nchini  Katika kupata majawabu ya changamoto zinaikabili  Jamii yetu Kwa Sasa .


Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia kizigo  akihutubia muhadhara katika Uzinduzi wa Utafiti uliofanya na shirika la RELI.

Katika utafati uliofanywa  katika wilaya ya Mpwapwa na shirika lisilo kuwa la kiserikali la   RELI   ambalo liliangazia  Katika masuala ya  kiwango cha uelewa wavijana Katika  viwango mbalimbali   ambapo utaffiti ulibaini  kati ya vijana 10 ni vijana wanne waliweza kuwa na uelewa wa kiwango cha Moja cha utatuzi wa changamoto amabacho ni kiwango cha chini kabisa.


Katika masuala ya kujitambua  utafiti ulibaini  asilimia kubwa ya vijana walionekana Kati ya vijana 10 ni vijana 5  walionekana kujitambua na Katika suala la heshima  ilibainisha asilimia 49.9% ya vijana  Wana heshima.


Aidha utafiti huo ulilenga kuanzia masuala makuu mnne ambayo  ilikuwa ni kuangalia ulewa wa vijana Katika  kujitambua ,ushirikiano,utatuzi wa matatizo na kiwango cha heshima Kwa Jamii.


          Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mount Igovu wakionyesha taarifa ya Utafiti iliyo fanywa na shirika RELI.



Alisema Katika kiwango cha heshima  vijana wengi wana uelewa wa kati  Katika kuheshimiana.


Akifungua utafiti huo Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia Kizigo Alisema Nchi zote zilizoendelea  zimetumia tafiti mbalimbali Katika kuondoa CHANGAMOTO za Jamii.


Hata hivyo alidai kuwa   serikali imekuwaikitumia tafiti zinazofanywa na tasisi zisizo kuwa za kiserikali.

           Baadhi ya Wazazi wakiriki katika uzinduzi wa Utafiti uliofanya na shirika la RELI juu ya masula yanayowahusu Vijana.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.