RAIS SAMIA ANAVYOPAMBANA NA MAADUI WA TAIFA UVCCM MPWAPWA.

 





Katibu wa vijana  wilaya ya Mpwapwa Isack Ngongi akiongea na vijana wa kata ya Ng'ambi  hawapo pichani.( Picha na Mpwapwa Habari )

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO wa Tanzania chini ya Rais wake Samia Suluhu Hassan wameendelea kupambana na maadui watatu wa Taifa hili kwa kuboresha huduma za Jamii zikiwemo Elimu Afya na umaskin wa Kipato.

Kauli hiyo hiyo imetolewa na Katibu wa jumuiya ya vijana wilayani Mpwapwa bwana Isack Ngongi alipofanya ziara ya siku moja katika Ng'ambi kuangalia. miradi ya Maendeleo na kuongea na vijana juu uundaji wa vikundi vya ujasilia mali, na ushiriki katika zoez la Sensa litakalo fanyika Agosti 23 mwaka huu.

Ngongi amesema viongoz wote kuanzia mwalimu Nyerere wamekuwa wakipigana katika Kuboresha huduma za Jamii "lakini Rais wa awamu ya sita ndio kapiga bao la tiktaka kwa ujenzi wa vituo vya Afya  katika kata nyingi ambapo akina mama wajawazito wanajifungulia karibu, na kusababisha kupungua kwa vifo vya akina mama na watoto na kufikia maelengo ya milenium 2025 na mkakati wa Taifa wa kupunguza vifo vya akina mama na watoto.

Aidha amedai ujenzi wa madarasa mengi kupitia fedha ya UVICO na kuondoa  ada kuanzia kidato cha nne hadi cha sita ," lakini katika kupambana na umaskini kuna mfuko wa Tasaf na mikopo isiyo na riba inayo tolewa na halmashauri zote hapa nchini " alieleza.

 Pia kuhusu vijana kujiunga na vikundi vya ujasilia mali aliwataka vijana kuacha kulalamika bali  kuweza kujiunga na vikundi vya kijasilia mali ili kuweza kupambana na changamoto za ajira hapa nchini. 

 Amedai ili kuweza kuchochoea Maendeleo endelevu vijana lazima wajitokeze mwenye zoezi la Sensa linalokusudiwa kufanyika ogosti 23 mwaka huu.

 Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Richard Mlimo amesema kuwa Kwa sasa wanafunzi wa kata hiyo hulazimika kutembea umbali wa kilomita 34 kutafuta elimu na baadhi yao hulazimika kuacha Shule kutokana na umbali pia wengine hupata Mimba kutokana na kupanga mwenye magheto.

Baadhi ya vyumba vya madarasa vya shule ya Sekondari ya Ng'ambi   vilivyo jengwa kwa fedha ya UVICO 19 .

 Amesema Serikali imetoa jumla ya shilingi 470 kwa awamu ya kwanza ambayo imefanikisha ujenzi wa sekondari ya kata hiyo ambayo imekudusudia kuondoa changamoto ya Elimu kwa Watoto wa kata hiyo ambao walikuwa wakifaulu na kwenda kusoma kata ya jirani  ya chunyu..

Milimo alisema pia kwenye kata hiyo kuna miradi mingi inayoeendelea  ikiwemo miradi ya mabwawa ya maji na viwanda kwa ajili ya kukuza uchumi na Maendeleo ya kata Ng'ambi..

 Naye Katibu wa jumuiya ya umoja wa wanawake UWT Wilayani Hapa Bi Amina Mwiru amesema kuwa kutokana na kupatikana kwa Shule hiyo kutawasaidia Watoto wa kike kufikia ndoto zao ambazo zilikuwa zinakwamishwa na Umbali ulio kuwepo hapo awali.

Mwisho.

 


 

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.