TAKUKURU WAJA NA MBINU MPYA ZA MAPAMBANO YA RUSHWA.



 

 

 

Mpwapwa



Uongozi wa Kata ya Mima na mkuu wa TAKUKURU WA pili kulia wakiwa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi  katika kata ya Mima.

WANANCHI wa kata ya Mima mkoa wa Dodoma wameipongeza Tasisi  ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wilayani Mpwapwa  kwa kuanzisha mpango  wa kuwafuata wananchi katika  maeneo yao  na kusikiliza kero zao zinaohusiana na masuala ya Rushwa na Utawala bora.

Mmmoja wa wananchi  wa kata hiyo bwana Mathias Cosmas ametoa pongezi kwa uongozi wa TAKUKURU wilayani hapa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika kta ya Mima.

Bwana Cosmas amesema mara nyingi  wananchi wanakuwa nakero zao  za kuhusiana na uongozi rushwa na utawala bora lakini wanashidwa kuzitoa kutokana na  umbali  au kuto kujua taratibu  za njisi ya kuwasilisha malalamiko hayo.

Bwana Mathias amedai kuwa  hatua hiyo itasaidaia Tasisi kupata taarifa nyingi kwa wakati na kuzitatua  papohapo  kusaidia kuokoa pesa ya serikali.

“Hata jina lenyewe linasema kuzuia  mngebaki  huko mkisubiri kuwakamata mambo yanakuwa wameharibika  au mradi umeisha ndo mnagundua mapungufu  kwa sasa lazima tulitambue tatizo mapema na kulishughulikia  kama wasemavyo kuwa lazima tushughulikie vyanzo vya tatizo na si matokeo” ameongea

Aidha mmoja wa wananchi  katika kijiji hicho Bwana Lameck Lenjima  amedai kuwa  kijiji  kero kubwa iko kwenye baraza la mogogoro la kata  ambapo baadhi wa wajumbe wamekosa  uaminifu na hivyo kushidwa kutoa maamuzi  kwa haki na kutishia kutokea kwa vurugu kati walegwa.

Pia ameiomba tasisi ya  hiyo kuweza kushughulikia haraka  chamnagomoto ya  baadhi ya nyumba za kituo cha afya  zilizo kuwa zimeungua  ili wananchi waweze kujua muafaka wa pesa  zao kutokana na Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa nyumba za wanganga na hivyo huwalazimu waganga kulala nje ya kituo na kusabisha usumbufu kwa  wagonjwa wa dharula usiku.

 Naye diwani  wa kata  bwana Bezaleli Mnyabwa amekili kuwapo kwa changamoto kubwa  ya malalamiko kutoka kwa baraza la migogoro ya kata kuto kufuata utaratibu na kuwaonea baadhi ya watu hasa wanyonge kitu alichosema kinaweza kusabisha  uvunjifu wa amani au mauwaji kwa wanao daiana .

Naye Bi Jeny Maswala alidai wananchi wa kata hiyo huwalazima kutembea umbali wa zaidi ya kilomita  30 kutafuta huduma za kimahakama  wakati kikogwe wa mika 88bwana  Elia Chuga aliiomba wazee wa kijiji hicho kuingizwa kwe Mpango wa Tasaf aili waweze kujikimu kimaisha.

Kwa upande wake mkuu wa TAKUKURU Wilaya hiyo  Bi Julieth Mtuy  amesema  wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kutoka vijijini  hasa  mengi ya malalamiko yanahusu migogoro ya ardhi  na maamuzi ya wajumbe kulalia upande mmoja.

 

Hata hivyo Bi Mtuy  alisema  wameamua kuwafuata wananchi vijini  ikiwa na lengo la  kuwajengea uwezo,kuwaelimisha na kujikita katika kuzuia sana kuliko kupambana zaidi.

“ Kwa sasa tasisi itakuwa inazunguka katika kata kwa kutoa Elimu,lakini  malalamiko mengi tunayoyapokea mengi yao  utakuta  labda ni kuto kujua utaraibu tu hivyo tunakuja kuwajengea uwezo  na kuwaelimisha lakini sio kwamba tumeacha kukamata kwanza tunazuia na kupambana  ikiona tumefikia kwenye mapambano ujue kuwa tumekuelisha tumekufundisha hukutusikiliza  sasa ndo tunaingia kwenye hatua ingine hivyo nawataka wanachi muendelee kutoa taarifa za ukweli na viongozi kuweza kufuata taratibuna kanuni za kazi zenu” ameongea  Bi Mtuy

Pia amesema  kwa  kuhusu suala la kituo cha Afya  Mima uongozi ngazi ya juu wanalifanyia kazi  na maamuzi yake yamefika hatua  ambayo  watapatiwa mrejesho siku si nyingi.

 

 MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.