DC MPWAPWA AMESEMA HAKUNA MTU ATAKAYE KUFA KWA COVID 19KAMA WATAZINGATIA MAELEKEZO YA WATAALAM.

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri  Akiongea na Mwandishi wa habari hizi ofisi kwake.
Picha na Mpwapwa Habari.



Na Stephen Noel .
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bwana Jabiri Shekimweri amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa CORONA CIVID- 19  na wasitishwe na mamneno ya mitandao juu ya ugonjwa huo.

Mkuu wa wilaya ameyasema hayo jana ofisi kwake akifanya mahojiani na  na mwandishi wetu juu ya mkakati wa wilaya thidi ya kujikinga na   maambukizi ya ugonjwa  huo ambao  kwa sasa umekuwa ni janga la kimataifa.

Shekimweri amesema  lazima  wananchi  waelewe na kuendelea kuchukua tahadhari thidi ya ugonjwa huo  ambapo kama “ kama wilaya tayari tumesha fanya uhamasishaji katika makundi yote yanayo tuzunguka  wakiwemo wafanya biasahara bodaboda  masokoni makanisani na misikiti juu ya kujenga uelewa kwa jamii na njia za kujinga   na kuwakinga wengine.
 Mganga mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Erichard Rwezahura  akiwa katika kanisa la Romani Catholic akifundisha wananchi njisi ya kujikinga na corona Hawaonekani pichani,

Pia mkuu wa wilaya hiyo amewataka wananchi kutafuta taarifa kutoka vyanzo sahihi  na vya kuamninika " acheni kamini mitandao wasikilizeni wataalmu wa faya ili kuweza kujinusuru”alisisitiza 

Tena amewaomba viongozi wa dini ,mila  na  kila mmoja kwa imani yake kumlilia mwenyezi Mungu  ili atuondolee janga hili la kidunia.

 Mganga mkuu wa wilaya hiyo Dkt Archard Rwezahura alisema kwa kuzingatia maelekezo ya serikali kupitia waziri mkuu tayari wamesha  tenga  maeneo ya kuwahifadhi wagonjwa hao kama watapatikana  na kila kitu cha afya kimetenga eneo maluum  kwa ajili ya wagonjwa hao kama watapatikana” aliongea  Dkt Rwezahura.

Pia Dkt. Rwezahura amesema lazima wananchi wa wilaya hiyo kuchukua tahadhari  pia lakini wasiwe waoga  sana waendelee kufanya kazi za kimaendeleo huku wakifuatilia maelekezo ya serikali  juu ya ugonjwa huo.

"Tukumbuke kuwa Mpwapwa sio kisiwa hvyo inaingiza wageni wasiopungua 150 kila siku  hivyo lazima tuchukue tahadhari yetu sisi wenywe tunao wahudumia  na tunao wapenda " aliongea Dkt Lwezahura.

Pia mmoja wa wa wanachi  wilayani hapo Bi Magreth Boma  amesema pamoja na ugonjwa huu kuingia nchini bado jamii haina uelewa mpana hasa vijijin juu kujikinga hasa kusalimiana Kwa mikono na wengine wakiamini kuwa wa Afrika hawapati ugonjwa huo.





Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.