Mwl.Augusta Lupokela kaimu mkurugenzi msaidizi wa mafunzo ya ualimu ,Wizara ya Elimu Sayansi na Tecknolojia.

MBUNGE wa Jimbo la Mpwapwa  Mhe George Lubeleje (Seniour MP) ameiomba serikali kuweza  kutenga Bajeti ya kutosha   katika sekta ya michezo  nchini ili  kuwezesha kuwezesha tanzania kufanya vizuri katika nyanja ya michezo  katika soko la ndani na nje ya michezo na ulimwenguni.
Mhe Lubeleje aliyasema hayo  juzi alipokuwa akifungua Kongamano la Michezo  la vyuo vya ualimu kanda ya kanda linalofanyika katiia chuao cha ualimu  kilichopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Mhe Lubeleje alisema kwa sasa  nchi ya Tanzania inashidwa kufanya vizuri katika nyanja za michezo kutokana na  serikali kushidwa kuwekeza vya kutosha katika sekta hii ya michezo  ambayo inaoneka kukua kwa kasi  hapa nchini.

Aidha amesema kwa sasa soko la michezo hapa nchini limeonekana kushika kasi kubwa na  kuwajumuisha vijana wengi na hivyo kwa kuona umuhimu huo serikali ya awamu ya tano imeamua kurudisha tena  michezo katika vyuo  ili kuweza kupata vijana  wenye viapaji vya michezo lakini pia kuwapata walimu watakao weza kufundisha michezo katika ngazi ya  shule za msingi na sekondari.

“ Kwa kweli kwa sasa Tanzania bado hatauajafanya vizuri katika mashindano  ya michezo  hapa nchini llakini yote hayo inatokana na serikali kushidwa kuwekeza vya kutosha  kwenye sekta ya michezo ikiwemo bajeti, miundo mbinu pamoja na vifaa  vya michezo  sasa nitajitahidi kushawishi bungeni  ili serikali iweze kutenga bajeti ya kutosha  katika sekta hii ambayo kwa sasa imebeba ajira kubwa ya vijana wetu” aliongea Lubeleje.
Kwa Uapnde wake  Kaimu Mkurugenzi msaidizi  wa mafunzo ya  ualimu kutoka wizara ya Elimu Sayansi  na Teknolojia  Bi Augusta  Lupokela alisema  alisema kuwa Chombo hicho kiliocho anzishwa miaka sabini iliopita kikiwa na lengo la kusimamia michezo  katika shule za sekondari na msingi kwa lengo kuweza kufanya vizuri  katika ngazi ya Taifa na ulimwengu mzima .

Hata hivyo  amesema  kuwa  chombo hicho kilifungwa  zaidi ya miaka 20 baada ya serikali kufuta michezo katika vyuo vya ualimu  lakini alisema “ kwa mimi  kama mwanamichezo pia naona fahari sana  kuwa michezo imerudi tena nikiwa  madarakani lakini lakini lengo kuu ni kuendeleza michezo katika ngazi ya sekondari na shule za msingi  hivyo lazima tufanye kwa tija ili tuweze kupata wanamichezo mahiri watakao weza kitangaza Tanzania katika ulimwengu wa michezo na Afrika mashariki.

Amesema UMISAVUTA   pia ilikuwa  pia kuwafunza zaidi walimu kimwili kiakili  kitaaluuma  na kimalezi yanaweza kumtambulisha mtanzania  popote atakapo kuwapo.

Pia amesema malengo mengine ilikuwa kuratibu na  kupima   michezo ya sanaa katika vyuo vya ualimu  Tanzania  ili kuweza kubaini  ipaji vya walimu katika vyuo  na kuendeleza sera ya michezo na sanaa  katika jamii ya Kitanzania .

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa  vyuo vya aulimu  kanda ya Kati  mkuu na chuo cha ualimu  Kinamapanda  Mwl , Maulidi  Hamisi  amesema   pamoja na serikali kurudisha  michezo vyuoni lakini bado shule za msingi na vyuo vinakabiliwa na changamoto kubwa ya maeneo ya pamoja na vifaa vya michezo , ambazo  alisema  vinaweza kutishia uendelevu wa michezo vyuoni .

Aidha Mwl. Maulidi ametumia  fursa hiyo kuiomba serikali  na wadau wa michezo kote nchini kuweza kuweza  kusaidia kauapatika na kwa vifaa   vya michezo  na serikali kuweza kutenga maeneo ya michezo  kwa ajili ya kuendeleza michezo hapa nchini .
 Kongamano hilo la siku  nne ambalo limejumuisha  vyuo vya ualimu Kinampanda , Bustani NA Chuo cha ualimu Mpwapwa  na mashinda kitafaifa yatanyika Mkoani  Lindi baada  ya kila kanda kupata  timu moja itakayo wakilisha kanda.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.