MAJI KIKWAZO CHA MAENDELEO IDILO WILAYA YA MPWAPWA


el-Mpwapwa
Wakazi  wa kijiji cha Idilo kata ya Mazae wilayani  Mpwapwa mkoani
hutumia maji yasiyo salama  na kutishia kupata magonjwa ya mlipuko
hasa kipindi hiki kuelekea msimu huu wa mvua za vuli.
Maji hayo yanayopatika  umbali km 2 hadi 3 kwa  pia ni maji ya
makorongoni ambayo  ni hatari kwa afya za wakazi hao.

Diwani wa kata hiyo  bwana Wiliam Vahae   amesema  wakazi hao
hulazimika kuamka alfajili na mapema ili kuwahi maji katika kisima
kabla hayajachafuliwa na wanyama  wa polini lakini kabla ya wafugaji
hawajanza kunywesha  Ng,ombe ambao wanakuwa na makundi makubwa ya
mifugo.
Aidha Vahae amesema kutokana na hali hiyo  kumepelekea wakazi wa
kijiji hicho kutumia maji ya visima vya asili na makorongo ambayo si
safi na salama na kutishia magonjwa ya mlipuko kama kipindupindi.

Amesema kufutia tatizo hilo tayari wakazi wa kijiji hicho wamesha
changa kiasi cha shilingi million 450,000/=ambazo ziko benki kwaajili
ya kusubiri nguvu ya serikali katika mradi huo mkubwa maji kijijini
kwao

Hata hivyo amesema baada  Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kuona
jitihada za wanachi hao  imetenga kiasi  cha shilingi milion 30 katika
 kipindi cha fedha mwaka 2017/2018 kwa ajili ya kuchimba kisima kirefu
 ambacho kitakuwa suruhu ya uhaba wa maji katika vjiji ya Idilo na
Kisokwe vya kata za Mazae.


Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Bi Agnes Masinjisa amesema tatizo la
maji katika kijiji hicho limekuwa la muda mrefu na baadhi ya
wanasaiasa waliligeza kuwa mtaji wao wa  kisiasa ili kuweza kupata
nafasi za uongozi.
 Bi Masinjisa amesema  wanapata usumbufu mkubwa  kutembea umbali mrefu
kwenda kutafuta  huduma hiyo  ambapo  akina mama na watoto ndio
wamekuwa  waathirika  wakubwa wa kero  hiyo  licha  kutembea  umbali
huo.
 Mtendaji wa kata ya Mazae bi Joina Machirika    amesema pamoja na
kijiji hicho kuwa na  mabomba ya maji yenye vyanzo ya mtiririko lakini
uharibifu wa mazingira umesababisha maji hayo kupungua na kuto kidhi
hitaji la wanachi kijiji hapo.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.