MKINZANO WA SHERIA KIKWAZO UHARIBIFU MAZINGIRA MPWAPWA.



 Na Stephen Noel. mpwapwa .
 MKUU wa wilaya ya Mpwapwa  mkoani Dodoma  bwana Jabir Shekimweri  amesema mkinzano mkubwa uliopo kati ya sheria mama ya mazingira  ya mwaka  2004 na  sheria ndogo ya halmasahauri ya wilaya hiyo ni miongoni mwa sababu zinazo fifisha  harakati za kupambana na uharibifu wa mazingira wilayani hapa.
Shekimweri ameyasema hayo mjini hapa alipokuwa akifanya mahojiano maluum majira juu ya hakarakati na mkakati uliopo kwa wilaya ya mpwapwa juu ya uharibifu wa mazingira  na matokeo yake.
 Shakimweri amesema kuwa  sheria ya mama ya mazingira  mwaka ya  mwaka 2004  inayo mtaka  mharibifu wamazingira  anapo patikana na hatia  anahukumiwa kifungo cha  cha miezi sita  hadi mika miwili jela au faini ya shilingi  50,000/= hadi  million 50,000,000/= au vyote viwili kwa pamoja.
Aidha amesema kuwa sheria ndogo ya halamasahauri hiyo inayo mtaka mharibifu wa mazingira   akipatikana na  hatia    anatakiwa kulipa faini ya shilingi 50,000/=na isiyo zidi shilingi 300,000/=  hivyo alisema kuwa wengi wao wametumia udhaifu wa sheria ndogo hiyo kuharibu mazingira  na kupelekea wilaya hiyo kuaanza kukubwa na matokeo ya uharibifu mkubwa  wa mazingiara hayo ikiwamo, mafuriko,kukauka kwa vyanzo vya maji, na upungufu mkubwa  wa mvua unaosababisha  Mpwapwa kuwa katika hatari kubwa ya kukabiliwa na jangwa.
Hata hivyo alisema  baadhi ya  makatibu wa kamati za migogoro ya kata wamekuwa wakitumia mwanya wa kesi za waharifu wa mazingira  kuwageuza kama mitaji ya kuendesha maisha yao kwa kuhongwa kitu kidogo na kuwaaachilia wakiendelea na uharibifu wa mazingira hayo.
Shekimweri alimtaka mwanasheria  mkuu wa halmasahauri kuweza  kuwashauri madiwani  wa halamasahauri hiyo kuweza kuifanyia malekebisho sheria ndogo hiyo ili iandane na  sheria mama ya mazingira  ya mazingira na  hali halisi ya uharibifu kwa wilaya ya Mpwapwa na matokeo yake.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.