POLISI MPWAPWA YAKABILIWA NA UHABA VITENDEA KAZI.










Na Stephen noel mpwapwa.
JESHI la polisi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma linakabiliwa na
upungufu  mkubwa wa vityendea kazi ikiwemo magari na pikipiki kitu
kinachopelekea jeshi hilo kushidwa kuwahi katika  matukio ya
kiuharifu.
Kauli hiyo  ilitolewa jana na Mrakibu wa polisi   bwana Paulo Ngonyani
mkuu wa kitengo cha Intelinjesia mkoani Dodoma  alipokuwa  katika
hafla ya kukabithiwa Pikipiki mbili zilizonunuliwa na wadau wa polisi
wa wilayani  Mpwapwa kwa lengo la kupambana  na uharifu wilayani hapa.
Bwana Ngonyani alisema katika jeshi la polisi limekuwa likilalamikiwa
sana na wanajmii kuwa wamekuwa wakichelewa kufika katika matukio ya
kiuharifu kutokana na kukabiliwa na chanagamoto kubwa ya ukosefu wa
vitendea kazi kama vyombo vya usafiri,pamoja na mafuta
Aidha Ngonyani  alisema  kwamba  ili kuimarisha dhana ya polisi jamii
wameamua kuwashirikisha wadau  wa maendeleo katika wilaya husika
kuweza kusaidiana kuzikabili changamoto zinazo likabili jeshi la
polisi kwa lengo la kukomesha uharifu katika jamii  na kuhakikisha
jamii inaishi kwa  amani  na utulivu.
Kwa uapande wake mkuu wa polisi wilayani Mpwapwa  marakibu wa Polisi
Bwana Hussen Mdoe  Mdoe alisema wilaya ya Mpwapwa inakabiliwa  sana na
uwizi wa mifugo,uuzaji na usamabazaji wa madawa ya kulevya  ya
sahambani na viwandani, uharibifu wa mazingira uwizi majumbani na
sehemu za biasahara pamoja  na vitendo vya watu kujinyonga au
kujeruana.
IMG-20161215-WA0006.jpg
Mkuu wa polis Mpwapwa akiongea kwenye hadhara ya kukbidhi pikipki
Mdoe alisema ili kuweza kufikia malengo ya kuifanya Mpwapwa iwe salama
lazima  wadau kushirikiana katika kuzitatua changamoto zinazo likabili
jeshi hilo katika  wilaya yake.
Pia alisema kutokana na Jografia ya  wilaya Mpwapwa  kuzungukwa na
milima  hivyo inawalazimu polisi baadhi ya maeneo  kutembea kwa mguu
kwenda kukabiliana na uharifu  sehemu ambapo gari haliwezi kufika kitu
alicho sema kinawachukua muda mrefu  na kusababisha kuchelewa kufika
katika matukio.
Mdoe alisema katika Mpango mkakati  wao ni kuweza kununua  pikipiki
kumi kwa kushirikana na wadau  ambazo zitawasaidia polisi  kufika
sehemu ambazo gari haliwezi kufika
Mmoja wa wadau wa polisi wilayani hapa Shekh Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa
 Mohamed Seif Sabaa aliiwataka polisi hao kuweza kuwa waaadilifu na
kuto kubambikia watu kesi  na kuachana na vitendo vya kuendekeza
rushwa ili kuwasaidia watu katika  matatizo yao.
Hata hivyo  Mgeni Rasmi katika  hafla hiyo  katibu tawala  wa wialaya
ya Mpwapwa Bi Atanasia Kabuyanja  aliwapongeza jeshi la polisi
wilayani hapo  kwa kuweza kusimamia Amani  japo na kukabiliwa na
chanagamoto lukuki.
Bi Kabuyanja  alisema  suala la kusimamia uharifu si suala la polisi
pekee bali aliwataka wanachi wote wa wialaya ya Mpwapwa kuweza  kutoa
taarifa ya vitendo vyote kiuharifu  vinavyoa ashiria 

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.