AUWA MKEWE KWA KIPIGO



  Na noel  Stephen  mpwapwa.
JESHI la polisi wilayani mpwapwa Kijana mmoja  aliyefahamika  kwa jina  la Hamis Nwage   kwa tuhuma za kupiga hadi kumuua mke   (mpenzi wake).
 Tukio hili lililotokea    asubuhi ya feb 11 katika eneo la hazina wilayani mpwapwa mkoani  Dodoma  ambapo kijana huyo  alimpiga hadi kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina Amana Makamba kwa kutumia kitu kianachosadikiwa kuwa ni kizito hali iliyosababisha mauti(37) .
Akiongea  mmoja wa mashuuhuda wa tukio hilo ambae ni dada wa marehemu  Bi  Stela  Mwasongwe  amesema  kuwa  siku ya tukio  walikuja kuambiwa na  majirani  kuwa   mdogo  wake anasadikiwa  kuwa  kapigwa  na kujeruhiwa na mume wake ndipo walipofika eneo hilo na kumkuta mdogo wake huyo akiwa amekwishafariki.
Mjomba wa marehemu  musa mhina   amesema kuwa   hajui kilichotokea  juu ya mtoto wao  bali  walikuja kuambiwa asubuhi  ya leo kuwa  mtoto wao  ameuwawa na mumewe   kwa tuhuma za wivu wa mapenzi .
AIDHA amedai kuwa  tangu kuanza kwa mapenzi yao  wao kama wazazi  walimkataza binti yao  kuolewa na   bwana huyo kutokana na kuwa bwana huyo  hutumia madawa ya kulevya  sana .
Mara baada ya kufanyia kitendo hicho cha mauaji mtuhumiwa alikunywa maji ya betri kwa lengo la kujiua lakini wasamaria wema walimuwahisha hospitali ya wilaya ya mpwapwa kkwa matibabu.
Kamanda wa polisi wilayani mpwapwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea juu ya tukio hilo.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.