KIJANA WA MIAKA 20 ABAKA MTOTO WA MIAKA 6 PWAGA MPWAPWA



Na noel Stephen mpwapwa 

 Kijana mmoja  aliye tambulika kwa jina Teophil Nganga(20)mkazi wa kijiji cha Pwaga  wilayani mpwapwa mkoani Dodoma  anashikiliwa na polisi  katika kituo cha polisi  Kibakwe kwa tuhuma za  kutaka kumbaka mtoto wa miaka  7 mwanafunzi wa chekekaea katika shule moja wapo ya kata  hiyo.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika kata ya  Lumuma   wilayani mpwapwa ambapo kijana  Teophil  anadaiwa  kumbaka  mtoto huyo  kwa kumdanganya kwa kutaka kumpa karanga  za kutafuna.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo na mwanaharakati  wa shirika la AFNET la  kuapmabana na vtendo vya ukatili wa kijinsia  katika kata hiyo Clemenc Ngewe  aliambia  mwananchi kuwa kijana huyo alimwita mtoto huyo kwa madai  ya kutaka kumpa karanga na  ndipo alipo mwingiza ndani ya  chumba chake na kuanza kumbaka.

Clemenc alisema baada ya mtoto huyo  kuingia ndani   walisikia kelele za mtoto  za kuomba msaada,  na ndipo walipo enda kutoa msaada walikuta mtoto huyo na  huku mtoto akiwa analalamika kuwa kambakwa.

Mganga mkuu wa kituo cha  Afya cha kata hiyo Mhawi ……….. alisema baada ya mtoto huyo kupelekwa katika kituo cha afya  hawakuona usahahidi wowote kwa mtoto huyo uchubuliwa ua  mabaki ya u chafu “hivyo tulishidwa kugundua kuwa kweli  mtoto huyo amebakwa au laa lakini maelezo ya mtoto yanadai kuwa  amebakwa  na kijana huyo ”alieza muhawi na kuongeza.

Aidha alisema baada ya tukio kutokea  wazazi wa mtoto huyo walimpeleka mtoto huyo kwenda kupima  wakati tayari amesha lala siku moja  na ameoga  na kuoga kitu ambacho kinapoteza ushahidi kabisa “lakini vipimo tulivyo pima  ndivyo tulivyo gundua  hivyo kwa hiyo hatupinagani na vipimo’’ alielezea zaidi muhawi.

Mzazi wa kiume wa mtoto huyo Walesi Chugwa  amekanusha kabisa kuwa mtoto wake hajabakwa bali walikuwa wanacheza tu na wenzake “ mimi nakuambia kuwa hajabakwa walikuwa wanacheza tuu na wezake ndipo nilipo waadhibu tu kwa viboko vichache tu lakini hajabakwa”aliezea mzazi wake wa kiume.
 Taaarifa zilizo  lifikia gazeti hili zimedai kuwa  wazazi wa mtoto huyo tayari walisha  malizana  (walilipwa na upande wa kijana aliyebaka) na ndio maana  hata walichukua muda mrefu kwenda kupeleka  katika vipimo lakini walifanya hivyo tu kutokana na shinikizo la wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.