AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIKA 30 JELA KWA KOSA LA KULIMA BANGI.







Bwana Odeni Mwikola   akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akisindikizwa kwenda kuanza  Maisha Mapya Jela .




Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu kifungo cha miaka thelani jela bwana Oden Mwikola (32) baada ya kupatikana na hatia ya kulima zao haramu la Bangi .

Kesi Hizo zilizo kuwa zinasikilizwa na hakimu mkazi bwana Pascal Mayumba wa mahakama Hiyo ya wilaya. 

Hakimu mayumba aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa Oden Mwikola alitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 11 kifungu kidogo cha 1(a)na(b)ya kuzuia madawa ya kulevya   sura 5 ya mwaka  2015 ambapo walilima shamba la Bangi lenye ukubwa wa  heka moja. 

Hata hivyo Mayumba  aliiambia Mahakama kuwa kesi hiyo iliyopewa nguvu na mashahidi 5 na vielelezo vitatu ikiwemo hati ya ukamataji, maelezo ya onto na taarifa ya mkemia mkuu iliyo thibitisha kuwa mmea ulio patikana Katika shamba la Bwana Odeni ilikuwa ni Bangi. 



Pia alisema kutokana na vielelezo na ushahidi uliopelekwa mahakanani bila Shaka yeyote na mtuhumiwa  alipatikana na hatia .Mtuhuiwa huyo alipo pewa nafasi ya utetezi alikuwa kimya na kuto kueleza chochote. 





Katika nafasi ya maombolezo na ndipo alipo itaka mahakama ipunguzie adhabu kwa kuwa ana majukumu na familia na watoto 4 wanamtegemea. 

Mwendesha mashitaka wa polisi bwana Stephen Masawa aliiomba mahakama itoe adhabu kwa kwa mtuhumiwa kutokana na madawa kuwa kero kwa  Wananchi na serikali pia  na madhara ya madawa ya kulevya yanayo weza kuadhiri nguvu kazi ya Taifa Pamoja na kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania Katika vita dhidi ya madawa ya kulevya. 


Hakimu Mayumba aliambia mahakama kuwa kwa sasa Bangi imekuwa tatizo Katika jamii yetu na madhara yake ni makubwa  ilipo kuweza kuokoa jamii na kizazi cha badae mtuhumiwa atafungwa kifungo cha miaka 30 Jela kutokana na vifungu vya  sheria namba 11kifungu kidogo 1 (a) na (b) sura ya 5 ya mwaka 2015  ya kuzuia madawa  ya kulevya.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.