VIJANA 4800 WAWEZESHWA MITAJI NA SHIRIKA LA BRAC MAENDELEO DODOMA


DODOMA,




Afisa tarafa ya Mpwapwa Bwana Obert Mwalyego  akimkabidhi mmoja wa wanufaika wa vifaa vya kufanyia kazi  vifaa vya saloon.



IMEELEZWA kuwa umaskini wa kipato  ni Moja wapo ya yanzo vikuu vya wasichana wengi  kufanyiwa ukatili wa kijinsia ndani ya jamii   tunamo ishi.

Kauli hiyo   imetolewa  na kaimu Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa ambae ni katibu tarafa  wa tarafa ya Mpwapwa Bwana Olbert Mwalyego  wakati wa sherehe za kukabithi vifaa vya kufanyia kazi Kwa  Mabinti barehe ambao walipatiwa mafunzo ya ujasilia Mali na kufuzu mafunzo hayo na shirika la black maendeeo.

Mwalyego amesema Kwa Sasa kundi kubwa linalo jikuta likiathiriwa na masuala ya ukatili wa kijinsia  ni kundi la vijana na Mabinti barehe ambao wengi wao ambao hawana ajira."ukweli ni kwamba tafiti mbalimbali zinadai kuwa moja wapo ya vyanzo vya ukatili ni umaskini wa kipato unaotokana na vijana wengi kukosa mitaji ya kufanyia kazi hivyo nawapongeza sana Black maendeleo  kwa kuwapatia vitendea kazi  mabinti hawa ambapo itapunguza kundi kubwa la vijana waliokuwa hawana ajira" alieleza.

Meneja wa mradi wa brac maendeleo wilaya ya Mpwapwa Bi  Alana Komba  amesema kwa wilaya ya Mpwapwa  Mabinti waliohitimu  mafunzo hayo Katika nyanja  ya biashara waliwezeshwa  vifaa kama Cherehani,vifaa vya saluni,nafaka nguo za mitumba,vifaa vya kupikia Friji na vitenge .

Naye meneja wa mradi wa Brac  mkoa wa Dodoma Bi Asia Botea amesema mradi   ulianza na Jumla ya washiriki Wasichana/ Wanawake na wavulana 4,800 katika mkoa wa Dodoma ikijumuisha wilaya ya Dodoma Jiji, Kondoa na Mpwapwa

".washiriki walio hitimu ni zaidi ya 3800 wengine walishindwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuhama makazi, kupata ajira na shughuli zingine za kimaendeleo na kutotaka kushiriki kwa hiari zao binafsi" alieleza Bi Botea
 

Mnufaika mwingine wa kata ya Chunyu  akikabithiwa cherehani kwa ajili ya kufanyia kazi.

Aidha amedai kuwa Washiriki zaidi ya 1600 ni wanafunzi walio nufaika kwa kuwezeshwa vifaa mbalimbali vya kurahisisha kubaki shuleni, vifaa  kama baiskeli kwa wanafunzi wanaosoma mbali, madaftari, mabegi na sweta za shule kulingana na uhitaji wao ambao alisema vifaa hivyo viliweza kupunguza utoo na kusaidia vijana wengi waliokuwa wakitaka kuacha shule kubaki shuleni.

Hata hivyo amedai mradi unawezesha wasichana wenye malengo ya kufanya biashara kwa kuwaongezea au kuwapa mitaji ya biashara wapendazo.

Amesema lengo la mradi shirika kufanya hivyo ni kuwainua kiuchumi na kuteketeza umaskini na ukatili wa kiuchumi  ambao umekuwa ni wimbi wanalokutana nalo wasichana na wanawake na kufifisha ndoto zao za kimaendeleo.

"Wasichana 1000 wa Mkoa wa Dodoma wanawezeshwa kwa kupewa vifaa vya Saluni, cherehani, mifugo, kilimo, nafaka, vitenge, vijora, balo la mitumba na vifaa vya mapishi ili waweze kujisimamia wenyewe kifedha na kuinuka kiuchumi."

Ameongeza kuwa kuwawezesha  kiuchumi kunaambatana na utoaji wa posho za kujikimu kwa wasichana waishio mazingira magumu (Kaya fukara) na  kuwatafutia masoko Ili kuweza kuendelea kuwapa elimu za biashara na usimamiaji fedha pamoja na kuwapa msaada wa haraka pale wanapohitaji kwa lengo la kuhakikisha wanaweza kuinuka kiuchumi kama lengo mojawapo la mradi.

Amesema zaidi ya Milion 500, zimetumika katika kuhakikisha walengwa wamewezeshwa kwa kiwango bora kulingana na uhitaji wao.
 
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii bwana Bahati   Magumula amesema  shughuli zinazofanywa na shirika la black maendeleo  zinamgusa Moja Kwa Moja  mwanamke na msichana lakini pia inasaidia sana kupambana na adui umaskini ambae ni Moja maadui wakuubwa taifa hili tangu tupate uhuru.

 

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.