ASASI ZA KIRAIA ZA LALAMIKIWA KUTO KFIKIA MALENGO.
Na noel Stephen Mpwapwa
I mebainika kuwa Asssi za kiraia nchini japo kuwa zimefanya kazi kubwa kwa jamii na serikali lakini bado hajijafikia malengo yanayo takiwa kutokana na rasilimali zilizo tumika na matokeo yanayo onekana.
H ayo yamebainishwa na Bwana AYUBU KUPONA afisa mipango kitengo cha Sera na Maendeleo katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl mjini Dar –ES-Salaam alipo kuwa akifungua warsha ya watendaji Wakuu wa AZAKI TANZANIA.
Bwana kupona alisema kuwa japo kuwa asasi nyingi zimefanya kazi nchini bado kuna changomoto ya kuyafikia malengo yaliyo kusudiwa ingawa pesa nyingi imetumika katika kitengo hicho kitu alicho sema kuwa matokeo haya endani na kiwango cha rasilimali zilizo tumika .
Aidha alidai kuwa asasi nyingi nchini bado hazijafanya kazi za kufuatilia mambo makuu ya kitaifa ili kuweza kuleta mabadiliko yanayo mgusa mlegwa wa hali ya chini TANZANIA.
Pia alidai kuwa yapo mabadiliko ambayo yanaonekana kwa jamii na kuleta matokea yanayo tia moyo bali alizitaka assi za kiraia kujitahidi kutumia rasilimali kidogo walizonazo ili kupunguza malalamiko ambayo hutokea kutoka kwa wadau na walegwa pamoja na serikali nchini.
Akiongea mmoja wa wanawarsha kutoka katika kituo cha wasaidizi wa kisheria IRINGA paralegal Bwana Sigfrid Mapunda alisema kuwa asasi nyingi nchini zimeshidwa kusimamia dhima na dira ya shirika kitu alicho kisema kuwa kinashusha utendaji wa shirika na kupelekea kushidwa kuyafikia matokeo yaliyo kusudiwa.
Pia wanawarsha hao kwa pamoja walidai kuwa watendaji wengi wa asasi wana uelewa mdogo juu mambo ya uongozi wa asasi kitu walicho kisema kuwakinapelekea kuwa na migogoro mingi ndani ya asasi nyingi hapa nchini.
Kwa upande wake Bwana STEPHEN LWITIKO mratibu wa mtandao wa mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali wilayani mpwapwaNGOMNET alidai kuwa udhaifu miongoni mwa katiba za mashirika kunapelekea kuwepo kwa muingiliano wa majukumu kati ya bodi ya ukurugenzi na watendaji wakuu wa Asasi.
Katika Warsha hiyo ambayo ilikuwa ya kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi ndani ya asasi wakuu hao waliweza kuainisha majukumu ya watendaji wakuu wa asasi ambapo alisema kuwa ni kubaini Dira, dhima, na malengo mahususi ya ASASi.
Mengine ni kuhakisha kuwa na uongozi wa sheria na uwajibikaji ndani ya Asasi na kubaini ,kufuatilia uwezo wa tasisi kuhusu huduma za program zake.
Comments
Post a Comment