AMUUNGUZA WIFI YAKE SEHEMU ZA SIRI.

KATIKA hali ya kushangaza na kusikitisha,mkazi wa moshi bar Manispaa ya Ilala,amedaiwa kumuunguza  wifi yake( 15) sehemu zake za siri  na kumsababishia maumivu makali.

Hayo yametokea jana Jijini Dar es Salaam, baada ya askari polisi wa kituo cha Stakishari, kupokea taarifa kutoka kwa majirani juu ya unyama huo aliofanyiwa binti huyo.

Polisi hao mara baada ya kupata taarifa hiyo, walifika nyumbani kwa mtuhumiwa lakini iliwachukua zaidi ya saa mbili kufanikiwa  kumtoa ndani mtuhumiwa ambaye alidaiwa kujifungia.

Hata hivyo, hali ilikuwa tete baada ya wakazi na majirani  wa eneo hilo walioguswa na tukio , walipoamua kuvamia nyumba hiyo baada ya kupokea taarifa za uongo kuwa mtuhumiwa hayupo  na kuamua kuwashinikiza polisi wamtoe au wajichukulie sheria mkononi.

Kufuatia mvutano huo, Polisi waliofika kumchukua mtuhumiwa , walizidiwa na kuamua kuondoka  kwa lengo la kwenda kuongeza nguvu kwa kuongeza askari na mabomu ya kurusha ili kuweza kuwatanya wananchi waliokuwa na hasira.

Licha ya kuongeza askari, haikuwa kazi rahisi kuwatawanya mpaka walipoamua kupiga risasi  hewani na kufanikiwa kuwatawanya wakazi hao waliokuwa na hasira sambamba na kumtoa mtuhumiwa aliyekuwa amejificha juu ya dari ya nyumba.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.