MKUU WA WILAYA AHIDI KUJIUZULU AKISHIDWA KUPAMABANA NA RUSHWA
Na Noel stphen mpwapwa ..
MKUU WA WILAYA ya Mpwapwa bawana CHRISTOPHER KANGOYE ameahidi na amesema yuko tayari kujuuzuru ukuu wa wilaya kama endapo atamkamata mtu yeyote na rushwa harafu huyo mtu asijukuliwe hatua za kisheria na vyombo vinavyo husika.
Bwana Kangoye ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wilayani mpwapwa alipo kuwa akifungua mjadala wa wazi wa Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Wilayani hapo mkoni Dodoma (PCCB)
Alisema kuwa yeye amekuja wilayani mpwapwa kwa ajili ya kuwatumikia wana mpwapwa na sio kutumikiwa na wana mpwapwa, hivyo alisema hapendi kusikia malalamiko ya wanancjhi juu ya kunyanyaswa na baadhi ya watendaji wa serikali na tasisi zake kwa kuombwa rushwa kwenye haki zao za msingi kama afya elimu maji na utumishi.
Aalisema kuwa umaskini haiuwezi kuondoka kwa kuendekeza rushwa na kufichaficha mambo kwa kulindana kwa baadhi ya watendaji wa serikali pindi mtu apatikanapo na tuhuma za rushwa au ubadhilifu wa mali za serikali.
Kwa upande wake kamanda wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilayani hapa Bwana Maiko Makoba alisema kuwa kuna tetesi nyingi na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya kulalamikia huduma wapatiwazo kwenye hospitali za serikali kuwa wananyanyaswa na kuobwa rushwa wakati wa kutaka huduma.
Pia Makoba alisema kuwa huduma ya afya lazima ipewe kipaumbelekwa wahudumu wa afya kufanya kazi kwa moyo ili wananchi wanapo patwa na malazi lazima wataenda kutibiwa hivyo kama watendeji wa afya wanaendekeza rushwa wanachi watanyanyasika sana na kupelekea kuichukia serikali iliyoko madarakani na kuitolea lugha chafu kitu alichosema kuwa lazima watendaji wa idara hiyo kuzingatia maadili na kanuni za kazi.
Katika mjadala huo wa wazi Bwana makoba aliwataka wanachi kutoa kero zinazojitokeza katika sekta ya afya ili wajirekebishe na kuweza kutoa huduma bora na zenye tija kwa jamii na walipa kodi
Akiongea mmoja wa wachangiaji katika mjadala huo aliye jitambulisha kwa jina la David Thomas alida kuwa huduma ya bima ya afya ya jamii haina tija kwa wanyonge; pamoja na kuwa na bima lakina ukienda hosptalini unaandikiwa dawa tatu unapewa moja na zingine unaambiwa ukanunue wakati jana tu gari la MSD limeshusha dawa iankuwaje kanma sio rushwa ni nini”?alihoji bwana Thomasi
AIDHA pia wananchi hao walisema kuwa wadi ya wazazi huobwa kila mzazi ajifunguapo huobwa tsh 5000/ ya asante na manesi na pindi akosapo hiyo hela hutolewa maneno machafu na matusi na kumkataza kumruhusu mpaka atoe hiyo hela./
Mjadala huo ulilenga kuwahusisha wananchi na wahudumu wa idara ya afya kuweza kuachana na rushwa na kutoa huduma kwa jamii ili kupata taifa endelevu na kufikia malengo ya mkukuta na malengo ya mileniamu.
KWA UPANDE WANGU NINGEPENDA VIONGOZI WAWE MAKINI NA KAULI WANAZO ZITOA MAANA AKIFIKA SIKU AKASHIDWA KUWAJIBIKA TUNAHITAJI AWAJIBIKE,LAKINI EWE MKUUU NI KWELI TNZANIA HII HATUANA TABIA YA KKUJIWAJIBISHA CHUKUA HATUA UWE WA KWANZA WEWE.
ReplyDeleteUKWELI NI KWAMBA HIYO NI MANENO TUU MBONA VIONGOZI WA JUU WAMEFANYA MAMBO MENGI NA MAKUU YA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA LAKINI WAMESHIDWA KUWAJIBIKA SEBUSE WEWE ANZA TUTAKUONA.
ReplyDeleteKWA KWELI TUZINGATIE UONGOZI NA UTAWALA BORA HAYO MABILIONI MNAYOYACHEZEA MNAYATOA WAPI? NA KWANINI UNAWEKA KWENYE AKAUNTI ZA NJE NA SIO MUWEKE AKAUNTI ZA HAPA TANZANIA
ReplyDelete