KUKAMATWA KWA BADWELI NI UTATA MTUPU

Kigoma Kusini, David Kafulila ameilipua Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) kuwa imekithiri kwa rushwa.

Kutokana na tuhuma hizo, Kafulila amemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuvunja kamati hiyo, vinginevyo yeye atajiondoa.

Pia mbunge huyo ameitaka Kamati ya Maadili kulitumia Bunge kumvua ubunge, Badwel, kutokana na tuhuma za kupokea rushwa zinazomkabili.

Kafulila alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari huku akisisitiza kuwa, wananchi hawatakuwa na imani tena na kamati hiyo.

“Ikumbukwe Juni 13, 2011 nilieleza bungeni namna wabunge wa Kamati ya LAAC wanavyoomba rushwa kwa watumishi wa Serikali, huku nikimtaja kwa jina Mbunge wa Bahi, Omary Badwel kuwa ni miongoni mwao,” alisema Kafulila ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi ya Takukuru, Alex Mfungo alisema juzi kuwa mbunge huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema hana taarifa zozote za mbunge huyo kukamatwa.

“ Sina taarifa za mbunge kukamatwa na Takukuru, kama ni kweli tutaletewa taarifa rasmi ndipo ninaweza kuzungumzia suala hilo,” alisema Makinda kwa simu.

Awali, Kafulila alisema licha ya kutoa taarifa hiyo bungeni na kumwandikia Spika kuhusu vitendo vya rushwa vya baadhi ya wajumbe, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

“ Nilijitoa mhanga kwa kutaja majina ya wabunge wanaoomba rushwa kwa watumishi wa Serikali, lakini hatua hazikuchukuliwa, sasa leo Takukuru wamemtia mbaroni mmoja wao, bado hamuamini,” alisema Kafulila.

“ Sasa naomba niweke wazi kwamba kama Spika hataivunja kamati hii na kuunda nyingine nitajiondoa kwenye kamati kwa sababu itakuwa imepoteza imani kwa wananchi,” alisema Kafulila.

Alisema kamati hiyo imepoteza uhalali na sifa za kuendelea kuzikagua hesabu za serikali za mitaa kwa sababu wajumbe wake wanatuhumiwa kwa rushwa.

Kafulila alisema ni wajibu wa Spika kutafakari upya kuhusu hadhi ya kamati hii na kuipanga upya kwa kuzingatia masilahi ya umma.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, ndiyo yenye jukumu la kusimamia hesabu za serikali za mitaa.

“Serikali legelege ni matokeo ya Bunge legelege kwa kuwa ni kazi ya Bunge kusimamia na kuidhibiti Serikali kikatiba,” alisema Kafulila.

Mbunge huyo wa Kigoma Kusini aliitaka Bunge kuweka azimio la kumvua ubunge Badwel kwa vitendo vyake vya rushwa.

“ Kamati ya Maadili ya Bunge ifanye hivyo ikiwa ni hatua za kinidhamu kuchukuliwa kwa mbunge huyo kwa tukio hilo la aibu,” alisema.

Kafulila alisema hata mabunge ya Jumuiya za Madola ambalo Tanzania ni miongoni mwao, huchukua hatua za kinidhamu za kuwavua wabunge wanaotuhumiwa kwa makosa ya aibu kabla ya mahakama hazijatoa uamuzi.

Kwa mujibu wa Kafulila, Bunge la Uingereza limeshachukua hatua za kuwavua ubunge watuhumiwa zaidi ya 59 ili kujenga imani ya wananchi kwa Bunge lao.

“Kwa hiyo nafahamu kwa kutumia azimio, Bunge lina uwezo wa kumvua madaraka mbunge yeyote ambaye amefanya vitendo vya aibu vya kuliaibisha Bunge,” alisema.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 71(1) (d) Mbunge anaweza kupoteza nafasi yake ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mbunge huyo wa Bahi, Badwel, na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi wote wa CCM ni miongoni mwa wabunge waliotajwa na Kafulila (NCCR-Mageuzi) katika Bunge la bajeti mwaka jana kwamba aliwakuta wakiomba rushwa kwa viongozi wa halmashauri ambayo hakuitaja.

Juzi saa 9.00 alasiri, Badwel alikamatwa na Takukuru akidaiwa kupokea rushwa kutoka kwa watumishi wa Serikali katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
#25 chriss 2012-06-05 16:06
wewe mbona unatia aibu sana
Quote
 
 
+1 #24 Mdau 2012-06-05 01:47
Sijui kwa nini watu wanalindana ki[NENO BAYA]. Zitto Kabwe aliposema bungeni kwamba Serikali imefilisika alishushuliwa na wabunge wa CCM. Juzi juzi serikali imesema inahangaika jinsi ya kulipa watu mishahara.
Chadema walipoibuka na first eleven ya ufisadi wakashambuliwa. Muda mfupi baadae waliokuwemo mle wakaumbuliwa, wengine wakafunguliwa mashtaka.
Kafulila aliwasema wabunge wenzie wanaodai takrima kupitia kamati za bunge alishambuliwa akaambiwa akae chini. Leo "Mheshimiwa" kadakuliwa akidai na kukamata mlungura.
Zitto Kabwe naye alipozungumzia mambo ya madini wacha afukuzwe bungeni kwa muda. Muda mfupi baadae aliyoyasema yakajiri.
Ni lini CCM watakapojifunza kwamba mficha uchi hazai?
Quote
 
 
0 #23 kam 2012-06-04 22:02
Nina wasiwasi na weledi wa watunga sheria wetu...
Quote
 
 
0 #22 Edmund 2012-06-04 21:43
kwa vile amekamatwa bac tuachie mahakama pia hao wengine nao cku ikifika watabainika.
Quote
 
 
0 #21 hhhdsa 2012-06-04 21:38
POLE KafuLILA KWA kutuhangaikia wananchi wako
Quote
 
 
+2 #20 kimwagu I.S. 2012-06-04 15:23
Bunge ni mhimili mmojawapo kati ya mihimili mitatu muhimu inayombeba mwana aitwaye NCHI.Mihimili yote hiyo imeundwa kwa mujibu wa SHERIA MAMA(KATIBA).TAKUKURU ni mojawapo ya chombo au Taasisi ya Umma iliyoundwa kisheria kwa lengo la kudhibiti na kupambana na rushwa nchini. Ni wajibu na jukumu letu watz kukiheshimu na kushirikiana nacho katika kutekeleza majukumu yake. Kama Mhe.KAFULILA aliwahi kumtaja Mhe.BADWELL kuhusika na uchafu huo basi ametoa mchango mkubwa sana na ushirikiano wa kutosha katika mapambano dhidi ya rushwa.TAKUKURU inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria hivyo si busara kuingilia uhuru wa utendaji kazi wa chombo hicho kwa utashi wa kisiasa badala ya kuzingatia sheria,kanuni na taratibu zilizopo.Hata Bunge linafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa jambo ambalo naamini hata Mhe.Kafulila analifahamu vizuri sana.Tupunguze munkali, tusubiri tuone nini kitaendelea mahakamani.
Quote
 
 
+4 #19 Magessa Mulongo 2012-06-04 15:09
Quoting rutashubanyuma:
kafulila naye aache ubabaishi na ubaguzi. yeye alifukuzwa uanachama NCCR MAGEUZI akakimbilia mahakamani ikawa kinga yake. Sasa naye badwel bado hata hajafikishwa mahakamani unadai avuliwe ubunge na siyo kusimamishwa hadi suala lake litakapokwisha. Ikumbukwe bunge lililopita akina pesambili alikuwa na kesi ya ya jinai lakini hakuzuiwa kwendelea na ubunge sasa huyu badwel tatizo liko wapi?

Au Pesambili alipendelewa............sahihi ni kusimamishwa ubgune lakini huwezi ukamvua ubunge kwa tuhuma tu ambazo mahakama inaweza ikamsafisha.....sasa ikimsafisha ndipo mtafidia vipi yeye na wapigakura wake..........tujifunze kuheshimu sheria hata kama kuna ushindani wa kisiasa.

Pole sana jamaa yetu,kumbe anakuhusu katika maisha yako ya kila siku,ila ndo hivyo ameshakamatwa na lazia sheria ichukue mkondo wake,avuliwe kabisa ubunge,hii haihitaji mahakama kuthibitisha kwani ni readhanded
Quote
 
 
0 #18 moses andarson 2012-06-04 13:47
kila penye uozo hapakosi harufu kwani ukizoea vya kunyonga vya kuchinja hauta viweza udhabu kali itolewe kwa wahusika wote wanaohusika na tuhuma za rushwa sikufukuzwa bungeni pia sheria zaidi ifuatwe wananchi wamechoka
Quote
 
 
-4 #17 ibrahim Muhigi 2012-06-04 13:45
Mh spika wetu namsifu yuko makini najua hawezi kuwapendezesha wote ,Huyu ametuhumiwa tusimuhukumu tuiachie mahakama ndipo tujadili kufukuzwa kwake bungeni tuache jaziba sheria itachukua mkondo wake
Quote
 
 
+4 #16 nicholaus 2012-06-04 13:03
MAKOFI WANAYOPIGA BUNGENI SI BURE, NI STYLE YAO YA KULINDANDA. SEASON OF DELIVERY IS COMING SOON.
Quote
 
 
+6 #15 JENGELA CHRISS 2012-06-04 12:35
Huo ndio uzalendo tuutakao watanzania,watu wenye nia mbaya na taifa hili hawafai kuwepo katika uongozi!!!
Quote
 
 
0 #14 mpayukaji 2012-06-04 12:21
makinda ni spika wa njombe sio wa bunge la tanzania.
Quote
 
 
0 #13 Borry 2012-06-04 12:07
Huo ni mfano hai wa jinsi wana-kamati za Bunge walivyo mafisadi ukiachia wasafi wachache kina Zitto na Mrema.Wabunge mafisadi hutokana na serikali ya mafisadi.Spika hawezi kufanya lolote kwani nae ni mmoja wao,namshauri Mh Kafulila afuate taratibu next time anapokuwa na ushahidi ili washikwe kwa wazi kama hivi.
Quote
 
 
+6 #12 HUMPHREY LABAN 2012-06-04 11:45
Kafulila safi sana nakuombea Mungu akulinde, nchi hii imeoza kaaaaatika uongozi lakini kwa uwezo mungu wataaibika na kuumbuana na wataangamia wote.
Quote
 
 
0 #11 mboni buhigwe 2012-06-04 11:26
mh!!!!!
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!



7000 symbols left


Banner
Banner
Banner

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.