BAJETI YATANGAZWA V2012 V2013

MwanzoContactsEmailHabari Kubwa
Bajeti  Send to a friend
Thursday, 14 June 2012 22:03
0digg
Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akionyesha begi lililobeba hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013, wakati akielekea kuingia katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Mussa Juma, Dodoma
SERIKALI jana ilitangaza Bajeti ya Sh15trilioni kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ambayo pamoja na mambo mengine, imelenga kudhibiti mfumuko wa bei kwa kutangaza kutoa vibali vya kuingiza chakula kutoka nje, huku ikiwabana matajiri kwa kuongeza kodi ya bidhaa zisizokuwa za lazima.Akisoma bajeti hiyo bungeni Dodoma jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alitangaza pia kwamba Serikali imepanua wigo wa Kodi ya Mishahara (Paye) na sasa itawagusa wafanyakazi wenye kipato cha kuanzia Sh170,000 badala ya Sh135,000 ya awali, huku ikirejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kutenga Sh7 bilioni kwa ajili ya kuchukua vijana 5,000.
Dk Mgimwa katika Bajeti hiyo pia alitangaza ongezeko la kodi za bidhaa mbalimbali, ikiwamo, bia, soda, sigara, juisi zinazoingizwa kutoka nje huku ikifuta msamaha wa ushuru wa bidhaa kwa magari kwa wote waliokuwa wananufaika na msamaha huo.
Alifafanua kwamba kodi ya vinywaji baridi imepanda kutoka Sh69 kwa lita hadi Sh83 na mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nchini kwa kiwango kinachozidi asilimia 75, imeshuka kutoka Sh425 kwa lita hadi 145 kwa lita.
Kodi ya mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, imepanda kutoka Sh1,345 kwa lita hadi 1,614 kwa lita.
Alisema kodi ya vinywaji vikali imepanda kutoka Sh1,993 kwa lita hadi Sh2,392 kwa lita, bia inayotengenezwa nchini kwa nafaka na ambayo haijaoteshwa, kodi yake imepanda kutoka Sh248 kwa lita hadi Sh310 kwa lita. Bia nyingine zote kodi imepanda kutoka Sh420 hadi Sh525 kwa lita.
Akizungumzia marekebisho ya ushuru kwenye bidhaa za sigara, Dk Mgimwa alisema zote zisizo na kichungi na zinazotengenezwa kwa tumbaku inayozalishwa nchini, kiwango cha angalau asilimia 75, kodi imepanda kutoka Sh6,820 hadi Sh 8,210 kwa sigara 1,000.
Alisema Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kwa tumbaku inayopatikana nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kodi imepanda kutoka Sh16,114 hadi Sh19,410 na sigara nyingine zenye sifa tofauti na makundi hayo, kodi imepanda kutoka Sh29,264 hadi Sh35,117 kwa sigara 1,000.
Alisema tumbaku ambayo ipo tayari kutengenezwa sigara (cut filler) kodi yake imepanda kutoka Sh14,780 hadi Sh17,736 kwa bunda la sigara 1,000 wakati ushuru wa cigars unabaki kuwa asilimia 30.

Gharama za simu juu
Katika bajeti hiyo, Waziri Dk Mgimwa alisema muda w

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.