MPWAPWA KUWA JAGWA BAADA YA MIAKA KUMI.,WATAFITI
NA STEPHEN NOEL MPWAPWA
Imeelezwa kuwa baada ya miaka kumi zaidi ya wakazi wapatao wapatao 150,000 laki moja na elfu hamsini wa kazi wa wilaya ya mpwapwa na kogwa wataokosa huduma za maji kabisa kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika vyanzo ya maji vya milima kiboliani na kwa kwamdyanga.
Hayo yamebainishwa na watafiti wa huduma za jamii za kituo cha utafiti na mifugo cha Tanzania kilichopo wilayani mpwapwa Mkoa wa dodoma kijulikanacho kama LITI – MPWAPWA.
Akiongea na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya mpwapwa amabae kwa sasa amehamia wilaya ya Karagwe Bi Darling Lwegasila mkuu wa chuo cha utafiti cha mpwapwa Dk, Devid Sindalo alisema kuwa kutokana shughuli za kibinadamu zinazo endelea katika vyanzo ya maji vilivyoko kwenye milima kiboliani Wilaya ya mpwapwa wakazi wake watakosa maji kabisa kutokana na kukauka vyanzo hivyo ambavyo ndilo tegemezi kwa wilaya ya mpwapwa na kongwa bila hatua za makusudi kuchukuliwa kimakini katika jambo hilo.
Aidha Dk, SINDALO alisema kuwa shughuli zinazo endelea katika milima hiyo ni kilimo, uchomaji moto, na shughuli za uchomaji mkaa katika maeneo yanayo zunguka vyanzo vya maji hayo.
Pia alisema kuwa mbali na matokeo hayo ya muda mrefu kutokea bali kuna matokeo ambayo mpaka sasa wilaya hiyo imenza kukabiliana nayo hasa katika kituo chake cha utafiti kilichopo liti mpwapwa.
Madhara ambayo yameanza kujitokeza kwenye kituo ni kupungua kwa malisho ya wanyama katika kituo hicho magonjwa ya mapafu kwa ngombe na mbuzi ambayo yote hayo husababishwa na joto kuongezeka nchini na magonjwa na kuongezeka kwa kupe wanao umma ngombe na kuwasababishia ugojwa wa ndigana.
Pia Dk alisema “ kwa wanasiasa waache kutumia siasa kwenye mambo yasiyo hitaji siasa kwa maana nakumbuka kulikuwa na mpango wa kuwa hamisha wavamizi katika maeneo hayo ya vyanzo vya maji lakini siasa ikaingilia kati na wale watu wakaachwa kulekule kwa ajili ya maslahi ya wanasiasa”alisema Dk,sindalo
Pia naye mkuu wa wilaya hiyo wa zamani Bi Lwegasila alitoa lawama kwa vyombo vya kiutendaji vya wilaya hiyo ikiwemo polisi na mahakama kuwa hawakuwajibika ipasavyo katika swala la kupigania mazingira katika milima kiboriani kwa kusema kuwa swala hilo lilikuwa na dalili ya rushwa kilicho pelekea kushindikana kwa swala hilo.
Naye Askofu mstaafu wa kanisa la ANGLIKANA MPWAPWA Askofu SIMON Chiwanga amesema kuwa katika kulishughulikia swala hilo ameamua kuanzisha mradi wa utunzaji utunzaji katika safu za mlima kiboliani kwa kupanda miti na kulejesha uoto wa asili kwa kuanzisha shirika lijulikalo kama LEAD FOUNDATION
.
Na mkuu wa wilaya mpwapwa amesema kuwa katika mapango wake wa kazi hiyo ndiyo itakayo kuwa ndiyo shughuli zake za awali hivyo ametoa wito kwa watendaji wake wote kuwa wakae mkao wa kazi yeye ametumwa kuwahudumia wanachi na kutatua kero, zao hivyo hajazoea kupindisha pindisha mambo “ nawaambia walio vamia hivyo vyanzo vya maji wakae tayari kuondoka kwa hiari yao wenyewe bila hatua za kisheria. kuanza kuchukuliwa”.
Comments
Post a Comment