WANANCHI WATAKA KUELIMISHWA KABLA YA MAONI YA KATIBA.
Na Noel Stephen -mpwapwa 19,05,2012 Wanachi jimbo la kibakwe wialayani mpwapwa wameomba swala la ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi katika mchako wakatiba lazima upewe kipaumbele ili kuweza kupata katiba yenye matakwa ya weanachi wote hapa nchini. Wito huo umetolewa jana na wananchi wa jimbo la kibakwe wilayanoi mpwapwa katika mdahalo wa katiba ulio fanyika katika ukumbi wa muleba , na uliandaliwa na mtandao wa mashiriaka yasiyo kuwa ya kiserikali wilayani mpwapwa NGOMNET(Non governmental oganazationMpwapwa nert work) Wakitoa maoni yao katika mdahalo huo wananchi hao walisema kuwa mchakato wa kuwa na katiba mpya ni mkubwa na tena umechelewa mno hivyo vingozi wanatakiwa kutoa kwanza elimu ya uraia kuhusu haki ya binadamu na katiba ya nchi ili kujenga Taifa lenye kuwajibika na kujua haki na wajibu wao kwa serikali yao...