SERIKALI YASHAURIWA KUWAPA KIPAUMBELE CHA AJIRA WALIMU WANAO JITOLEA KWANZA.
Baadhi ya wanachuo wa chuo cha ualimu hapa Mpwapwa.
SERIKALI imeshauriwa kuweza kuwapa kipaumbele walimu waliohitimu nmafunzo Yao na wakaamua kujitolea Katika shule mbali mbali hapa Nchini Ili kuweza kuziba pengo la upungufu wa walimu Katika shule za Msingi na sekondari
Ushauri huo ulitoleaa na mdau wa Elimu na mbobezi wa masuala ya Elimu hapa Nchini
Mwl Dkt ,Wiliam Hugo Ndipo alipokuwa akiongea na chombo hiki Nyumbani kwake mjini Mpwapwa (Mji mpya).
Dkt Ndimbo alisema kwa sasa shule nyingi hapa Nchini zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu hasa shule za vijijin kabisa japo kuwa vyuo vy kati na vyuo vikuu vikiendelea kutoa wahitimu Kila mwaka .
Alisema " kiukwel kila mwaka vyuo hivi bimeendelea kutoa wahitimu wa vyuo vya kati na vyuo vikuu lakin upungufu Bado upo na hivyo husabanisha utoaji wa Elimu kuto kuwa SAWA kati ya maneo ya mjini na vijijin ,lakin hawa walimu wanaenda wapi mala baada ya kuhitimu wapo ambao wamejiajili ,wapo walio ajiliwa shule binafsi na wapo wanajitolea Katika maeneo wanako toka" alieleza
Ila pamoja na baadhi ya walimu kujitolea lakin inasikitisha pindi Ajira zinapotoka utangaaa waliokuwa wanajitolea pamoja na kuwa na vigezo hukosa nafasi wale wengine walikuwa labda kwenye Ajira binafsi au shule binafsi ndio hupata nafasi kwanza kitu kinacholeta ukakasi wa uzalendo na utu Kwa wale wanao jitolea" alieza zaidi
Alisema ili kuweza kurudisha uzalendo na usawa lazima wanaojitolea wapewe nafasi kwanza " Tena wapewe maeneo Yale yale wanayojitolea Ili kupunguza gharama Kwa serikali pindi wakipangiwa maeneo mengine na kusumbua kutaka kuhama baada ya muda mfupi .
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolijia Prof Aldolf Mkenda.
Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inaeleza kuwa hadi Februari, 2023 ilikuwa na uhitajii wa walimu katika shule za msingi ni 362,189 kwa kutumia uwiano wa 1:45 (Mwalimu mmoja kwa wanafunzi 45).
Hata hivyo walimu waliopo ni 175,864 ambao wanafundisha wanafunzi milioni 12.36 waliopo nchi nzima katika ngazi hiyo ya elimu. Hiyo ni sawa na kusema kwa wastani, mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi 70.
Uwiano huo uko juu kuliko mapendekezo ya Serikali ya mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi wasiozidi 45 katika darasa moja.
Ili kuziba pengo hilo wanahitajika walimu 186,325 au sawa na asimilia 51.44 au zaidi nusu ya walimu waliopo sasa.
Shule ya MsingWanafunzi wa i moja wapo Mpwapwa.
Pia, mahitaji ya walimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa shule za msingi ni walimu 4,462 ambapo waliopo ni 1,517 na upungufu ni walimu 2,945 sawa na asilimia 66.
Hata wakiajiriwa walimu wote hao, tatizo la uhaba wa walimu katika shule za msingi linaweza lisiishe kabisa kwa sababu kila mwaka idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza wanaondikishwa inaongezeka
Tatizo la uhaba wa walimu siyo tu la shule za msingi bali linazikumba hata shule za sekondari hasa zinazomilikiwa na Serikali.
Tamisemi inaeleza kuwa mahitaji ya walimu kwa shule za sekondari hadi kufikia Februari mwaka huu ni 174,632.
“Waliopo ni 84,700 na upungufu ni walimu 89,932 sawa na asilimia 51.5. Mahitaji ya walimu kwa shule za Sekondari yanatokana na masomo yanayofundishwa,” amesema Waziri Kairuki.
Wachambuzi wa masuala ya elimu akiwemo Richard Mabala wanasema uhaba wa walimu unawakosesha fursa wanafunzi kupata maarifa kwa ukamilifu kuwawezesha kufaulu mitihani yao na kupata stadi muhimu kuboresha maisha yao.
Mwisho.
Comments
Post a Comment