TAFADHALI MADAKATARI ,VIONGOZI MSIYAPUUZE


MIONGONI mwa habari zilizopo ukurasa wa mbele wa gazeti hili, ni tishio la Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) la kufanya mgomo usio na kikomo wiki mbili zijazo, iwapo serikali itashindwa kuyapatia ufumbuzi madai yao ya msingi, ikiwemo nyongeza ya mshahara.
Tumeshtushwa na tishio hilo kwa kuwa bado hatujasahau madhara yaliyotokea wakati wa migomo ya Januari na Machi mwaka huu, ambapo watu waliokwenda kwenye hospitali, zahanati na vituo vya afya vya umma kupata matibabu na huduma nyinginezo hawakuzipata.
Wapo watu waliopoteza maisha, waliopata vilema vya maisha na athari nyingine nyingi ambazo mpaka hivi sasa serikali imeshindwa kutaja migomo ile iliathiri kwa kiwango gani sekta ya afya.
Tunaamini kuwa, tishio hili la madaktari linaweza kufanyiwa kazi kabla ya wiki hizo mbili ili kuepusha hali kama ile tuliyoshuhudia huko nyuma, ambapo pia baadhi ya viongozi na watendaji wa walisimamishwa kazi huku wengine wakipoteza nyadhifa zao.
Kwa mujibu wa Rais wa MAT, Dk. Namala Mkopi madaktari wamekutana jana kupata mrejesho juu ya kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kufuatilia madai ya madaktari, lakini wameikataa ripoti yao.
Madai ya madaktari hao ambayo serikali imeeleza kushindwa kuyatekeleza katika mwaka huu wa fedha hadi katika bajeti ya mwaka 2013/2014, ni pamoja na kuwalipa posho, ikiwamo za kulala kazini walizodai tangu mwaka 2004 ambazo hazijawahi kubadilika kutoka kiwango cha sasa cha sh 10,000 licha ya mwongozo wa serikali kuelekeza walipwe kwa nusu ya fedha ya mkoa husika.
Madai mengine ni kulipwa posho kwa wale wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi yanayoweza kuwaambukiza magonjwa na kuwasababishia athari mbalimbali, ili iwatie morali.
Pia wanadai kulipwa posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu, kupata posho kwa ajili ya usafiri au mkopo wa gari, kupatiwa nyumba za kuishi, kuboreshewa mishahara yao, posho ya uchunguzi wa maiti na kupatiwa bima ya afya wao na familia zao.
Sote tunatambua umuhimu wa madaktari, lakini ni vema meza ya majadiliano ikatumika kutatua matatizo yaliyopo kwenye sekta hiyo kuliko kufanyika kwa mgomo ambao huathiri zaidi wananchi.
Tunasema hivyo kwa kuwa viongozi na watendaji wa serikali hutibiwa nje ya nchi, hivyo athari za hudumu mbaya zipatikanazo kwenye hospitali, zahanati na vituo vya afya hawazijui.
Tunaiomba serikali iache tabia ya kusubiri mpaka mambo yaharibike ndipo ikae chini na kuzungumza na wahusika, huu si wakati wa kucheza na maisha ya wananchi ambao ndio wanaotoa fedha kwa ajili ya kuendesha nchi.
Chonde chonde tunaziomba pande zote mbili zinazohusika na mgogoro huu kutumia busara na hekima kutatua tofauti zilizopo.
Tusingependa madaktari wafanye kazi kwenye mazingira hatarishi, yasiyo na vifaa, mishahara midogo, lakini mambo hayo yote yanaweza kutatuliwa kama serikali itakuwa na dhamira ya dhati ya kuboresha sekta ya afya.
Ahadi na maneno matamu yasiyotekelezeka vinavyotolewa na serikali kwa wafanyakazi wake, hazipaswi kupewa nafasi wakati huu ili kunus

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.