MATATANI KWA DAWA ZA DILI

Na  noel  Stephen Mpwapwa

Jeshi la Polisi Wilayani Mpwapwa Linamshikilia mfanya biashara mmoja wa kijiji cha Ng’hambi Bwana  Jeremia mhogo  kwa tuhuma za kukamatwa na dawa za kutibu binadamu    na  baadhi ya dawa hizo zikiwa na nembo ya MSD  kinyume na sheria.

  MKUU wa polisi  wilayani mpwapwa  Bwana  JEREMIA SHILA  ametibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema mtuhumiwa bado anashikiliwa na polisi lakini kwa sasa yuko nje kwa dhamana .

Bwana Shila  alisema kuwa  mtuhumiwa huyo alikamatwa na maafisa AFYA  WA WILAYA   walio enda  kufanaya uchunguzi katika eneo hilo na ndipo walio  mbaini mtuhumiwa huyo na alisema kuwa  maelezo mazuri anayo bwana afya wa wilaya   Bwana Plaivate Lweimamu amabae alikuwa ndiye mkuu wa msafara siku hiyo na kuwataka waandishi kwenda  kwa Bwana afya kupata maelezo kwa bwana AFYA HUYO.

  Akiulizwa bwana LWEIMAMU  kuhusu tuhuma hiyo  bwana Afya  huyo   aliwafukuza  waandishi wahabari kwa madai kuwa  waandishi hao waandike  walivyo sikia  na kuwa  yeye sio msemaji mkuu  hivyo yeye hashughlikii  majungu.

Akiulizwa kuhusu tuhuma  hizo Mkugurugenzi Mtendaji wa  halmashauri  ya wilaya ya  ya Mpwapwa Bwana FANUEL SENGE hakutaka  kulisemea swala  hilo na kutaka   waandishi wa habari  wasiliiandike swala hilo kwa madai kuwa watapoteza  uchunguzi  kwa mtuhumiwa ili polisi  wachunguze vizuri.

Chanzo  chetu cha habari kimedai  kuwa  mfanaya biashara huyo amabae hufanya biashara  ya kuuza  vyakula  na sio kuuza  madawa na pia kimedai kuwa  huenda  dawa hizo hutoka katika vituo vya afya zahati au mahospitali na huzinunua dawa hizo kwa bei nafuuu na kuziuza kwa wananchi kitu walicho hoji kuwa huenda  kodi zao kutumiwa vibaya na viongozi wachache wanopenda kujitajirisha kwa kuuza madawa ya vituo  za serikali kinyume na sheria.

 Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji hicho bwana Joel Kabwiga  alikili kutokea kwa tukio hilo hapo kijijini na kudai kuwa swala hilo liko polisi kwa uchunguzi zaidi na kudai kwamba  anacho kifahamu ni barua iliyo enda ofisini kwake na kumtaka bwana  Jeremia kuendelea na biashara zake na kuachana na biashara  ya vitu ambayo haviko kwenye leseni yake.

 Tukio hili limeonekana kupigwa  danadana  kwa wafuatiliaji  wa swala hilo japo kuwa  hutujui kinacho endelea lakini  huenda  ufatiliaji huo  dhaifu  utapelekea wananchi kuelewa kuwa kuna kitu katikatika ambacho  hupelekea swala hili kuendelea kupigwa danadana.




.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.