MOVEMENT ZA CHADEMA HATARI KWA CHAMA TAWALA
0 digg Elias Msuya CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezindua harakati za mabadiliko hivi karibuni jijini Dar es Salaam unaojulikana kama ‘Movement for change’ (M4C)’ wenye lengo la kuchukua nchini mwaka 2015. Katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Jangwani, viongozi wa Chadema wamefafanua maana ya harakati hizo, wakisisitiza kuingia Ikulu 2015. Akizungumzia kampeni hiyo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema kuwa kuna gharama kubwa kuiondoa CCM madarakani. “Kila mwananchi anawajibu wa kubadilisha maisha yake. Kila mtu anapaswa kuwa wakala wa mabadiliko. Kuiondoa CCM kuna gharama kubwa, kule Arumeru walichanga thumni zao na kila walichokuwa nacho na hatimaye tulishinda, au siyo? Tusije tukapata viongozi kwa fedha chafu” amesema Mbowe. Ili kuhakikisha kuwa chama hicho hakiingiliwi na mamluki, Mbowe pia amesisitiza kuwa watakuwa makini na wanachama wapya wanaohamia Chadema akisema kuwa watatakaswa kwanza kabla ya kupewa uanachama. “Kuna ...