POLISI WAJIPANGA KUUKABILI UHARIFU
Na Omana Gouth MPWAPWA
Jeshi la polisi wilaya ya mpwapwa linakusudia kutekeleza miradi miwili kwa kuwashirikisha wananchi kwa kuanzisha mtandao wa kiusalama na mpango wa akiba ya mafuta kwa lengo la kukabiliana na uharifu wilayani humo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa polisi wilaya ya Mpwapwa Bwana Jeremia Shila katika kikao cha baraza la madiwani kilicho fanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilayani Mpwapwa mkoa wa Dodoma
Pia alisema katika eneo la Mpwapwa lazima waondokane na mifumo ya kizamani wa ulinzi wa kutegemea baiskeli na kutembea kwa miguu, na sasa wanaingia katika mfumo wa kutumia pikipiki kwa kila kijiji na kata.
Akizungumza kwenye kikao hicho Bwana Shila alisema kila kijiji kitapatiwa pikipiki moja na kata kupewa pikipiki moja ya polisi kata, na vijana wawili kupatiwa mafunzo kwa kila kijiji na pia kupatiwa mawasiliano ya simu ili kurahisisha dhana ya polisi jamii.
Aidha alisema mpango huu utasaidia endapo tukio la uhalifu likitokea katika kijiji kimoja wana mtandao wa ulinzi toka vijiji vingine na polisi kata wakipatiwa taarifa wataenda haraka kutoa msaada katika eneo la tukio.
Pia alidai kuwa tafiti nyingi zimefanyika zinaonyesha kwamba jambo linalofanywa mara kwa mara ndilo linaweza kufanikishwa kwa sasa muda mwingi tunatumia kutafuta mafuta ili kufanikisha mambo mengine ya kiulinzi na usalama katika wilaya ya mpwapwa.
“Tumeamua kuandaa Harambee ya kuchangia akiba ya mafuta kwa kuwahusisha madiwani na wadau mbalimbali wa ndani ya nchi na nje ya nchi ya Wilaya ya Mpwapwa ili kufanikisha malengo tuliyoyapanga yatimizwe na kutekelezwa”alisema Shila.
Alisema kuwa fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo zitabadilishwa kwa lita za mafuta na kituo cha mafuta watakachoingia mkataba nacho siku hiyo ya tukio na kufanya kuwa mpango huu kuwa endelevu ili kuhakikisha muda wote polisi anakuwa na mafuta ya kutosha ili waondokane na polisi kuwa washuhudiaji wa matukio bali wawe watatuaji wa matukio.
Alisema kuwa mpango watakao anza nao ni juu ya oparesheni mbalimali za usalama kama ulimaji bangi , uuzaji wa pombe haramu ya gongo, na Siraha zinazo milikiwa kinyume cha sheria ili kufikia lengo la dhana ya utii wa sheria bila shuruti kitu alicho kisema kuwa kianzie kwa viongozi wenyewe.
MWISHO.
Comments
Post a Comment