ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPIGWA NA TEMBOOMANA
Na OMANA GOUTH MPWAPWA
Mtu mmoja anayejulikana kwa jina Baraka mlowe (25) mkazi wa kijiji cha pwaga kitogoji cha ikulu wilayani mpwapwa mkoa wa Dodoma amejeruhiwa na tembo na kupasuliwa tumbo hadi utumbo kuwa nje ya tumbo lake.
Akizungumza na waandishi wa habari kaka yake majeruhi bwana Geofrey Mlowe alisema kuwa siku ya tukio majeruhi alikuwa na nyumbani na alisikia kuwa tembo wameingia mashambani na wanaharibu mazao na ndipo alipo enda kuangalia hali ya shamba na kuwafukuza wanyama hao,
Alisema kuwa ndipo alifika mashambani alikuta tembo hao na alikuta watu wengi wakiwa wana shangaa tembo hao lakini yeye alitaka kuwashangaa kwa karibu ndipo tembo huyo alimrukia na kumwangusha chini na kuanza kumkanyaga na alimchoma na mkonga na ndipo alimtoboa sehemu za tumboni na kumtoa utumbo ukiwa nje.
“Alipo kuwa amekamatwa na tembo huyo watu wakapiga kelele na za kuomba msaada na ndipo tembo huyo alimuachia huku akiwa katobolewa utumbo na kuvunjwa mguu wa kushoto chini ya goti kwa kukanyagwa’’alisema bwana Mlowe.
Mganga mkuu wa hospitali hiyo Dk.MOHAMED PATHAN wa hospitali ya wilaya ya umedhibitisha kuwepo kwa majeruhi huyo na alisema kuwa atatoa taarifa ya maendeleo yake hapo baadae watakapo mfanyia uchunguzi kwa kina “ninchoweza kusema kwa sasa ana hali mbaya subiri tufanyie uchunguzi ndipo nitakapo toa majibu ya maendeleo yake”alisema dk pathan
Kaimu afisa wanyama poli wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Oska Malima alikili kuonekana kwa tembo katika maeneo ya kijiji hicho na alisema kuwa siku tatu kabla tembo hao walionekana katika kijiji cha makutupa laikini hawakuleta madhara yeyote, ila kinacho onekana tembo huyo anae jeruhi watu inasadikiwa kajeruhiwa na watu hivyo wanyama hao walionekana kujihami na watu wanaonekana kutokea mbele yake.
Pia alisema kuwa tembo hao walionekana wakiwa wanne na wametorsssoka kutoka hifadhi za wanyama za luaha mbuyuni mkoni iringa ambapo ni mpakani na wilaya ya mpwapwa
Aidha alisema kuwa sehemu wanamopita tembo hao inaonekana siku nyingi humo ilikuwa njia za tembo hao hivyo ni tabia ya tembo kurudia njia zao za zamani.
Na aliwataka wananchi wote wa wilaya ya mpwapwa welewe wanyama poli kwani wanyama poli wasipowachokoza hawawezi kuzuru mtu wa aina yoyote na kuwataka kuto kwashangaa kwa karibu zaidi ili waweze kujilinda ..
Comments
Post a Comment