GAZETI LA MWANACHI LAPONGEZWA


Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philip Mulugo akiwapongeza baadhi ya Wanafunzi wanne kati ya 100 wa Mpango wa Elimu wa Paa na Mwananchi wakati hafla ya kuwakabidhi hati za ufadhiri wa Masomo iliyofanyika kwenye Ofisi za MCL zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix
Ibrahim Yamola
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amezitaka kampuni mbalimbali nchini kuiga mfano wa Mwananchi Communications Limited (MCL), kwa kutoa udhamini kwa wanafunzi nchini ili wapate elimu.
MCL, kampuni inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen imeanzisha mpango maalumu wa kusaidia ukuaji wa elimu kwa kuwafadhili wanafunzi katika shule za umma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ikianza na wanafunzi 100 kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania.Akizindua mpango huo katika Ofisi za MCL, Tabata Dar es Salaam jana, Waziri Mulugo alisema hatua hiyo ni ya kuigwa kwani Serikali haiwezi kufanya kila kitu bila msaada wa sekta binafsi.
“Kitendo ambacho leo (jana) MCL mmekionyesha kwa jamii na Serikali, kinatakiwa kuigwa na kampuni nyingine ili kuinua kiwango chetu cha elimu hapa nchini,” alisema Mulugo na kuongeza:
“Kampuni binafsi, mashirika ya dini... tujikite katika kuhakikisha tunasaidia Serikali kama wenzetu wa MCL walivyofanya kwa kuwadhamini wanafunzi ambao hawana uwezo wa kuendelea na masomo yao.”
Alisema kitendo hicho cha MCL kuamua kuwasomesha wanafunzi hao ni cha kijasiri kwani wangeweza kutumia kiasi hicho cha fedha kuongeza mishahara ya wafanyakazi wake au shughuli nyingine lakini imeamua kukitoa kwa wananchi tena wa hali ya chini.
“Fedha hizi mngeweza kuwaongezea wafanyakazi wenu, kwani sidhani kama mishahara yao inakidhi, lakini hata kusaidia sekta nyingine kama afya, umeme, maji... lakini mmediriki kurudisha kwa wananchi kiasi kidogo cha fedha mnazozipata, kitu ambacho ni kizuri,” alisema Mulugo.
Ili kuhakikisha kuwa malengo ya mpango huo yanafikiwa, Mulugo alisema Serikali itahakikisha kuwa wanafunzi hao 100 watakaofadhiliwa na MCL wanasoma katika shule za bweni ili kuwarahisishia kusoma kwa ufanisi.
Awali, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni Mama ya MCL, Nation Media Group (NMG), David Maingi alisema mpango huo ambao ulianza miaka mitatu iliyopita kwa nchi za Uganda na Kenya, unazunguka katika nchi zote za Afrika Mashariki.
Maingi alisema mpango huo umekuwa ukiboreshwa kila mwaka na miaka ijayo utakuwa mkubwa na wenye ufanisi wa kutosha kwa wanafunzi wa kutoka nchi zote za ukanda huo.
Mbali ya kusoma alisema mpango huo utatoa fursa kwa wanafunzi wa mataifa hayo kusafiri nchi mbalimbali na kukutana kubadilishana mawazo lengo likiwa kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi wazuri baadaye.“Mwaka jana wanafunzi walikutana Kenya na kwa mwaka huu kuna uwezekano wakakutana hapa Tanzania. Mpango huu, utakuwa ukizunguka kila nchi,” alisema Maingi.
Alisema mpango huo utawasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wasio na uwezo, kuendelea na masomo na hatimaye kuja kuwa viongozi kwa siku zijazo.
“Udhamini huu utahusu ada ya shule, sare kwa mwanafunzi, vitabu, madaftari na mahitaji mengine muhimu ya mwanafunzi wakati wote akiwa masomoni,” alisema Maingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando alisema kampuni yake itafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba wanafunzi hao wanatimiza malengo ya mpango... “Itakuwa ni jambo la kusikitisha kusikia kwamba mwanafunzi tunayemfadhili anaharibikiwa akiwa kidato cha tatu.”
Kuhusu mpango huo, Mhando alisema: “Hautaishia mwaka huu pekee bali, utakuwa endelevu kwa kila mwaka. Tutawachukua wanafunzi kutoka kote nchini wasiokuwa na uwezo kutokana na kuwa yatima na kuwasomesha.”
Mmoja wa wazazi ambao watoto wao wamepata ufadhili huo, Hawa Balozi alisema kitendo ambacho MCL imekionyesha ni mfano wa kuigwa na watu wengine.
“Kitendo hiki mlichoamua kufanya ni cha kijasiri sana, hivyo namwomba Mungu awaongoze na kufikia malengo yenu,” alisema Balozi.
Mchakato wa kuwapata wanafunzi hao 100 katika mpango huo wa Paa na Mwananchi ulianza Aprili 2, mwaka huu kwa washiriki kutuma maombi yaliyokuwa yakimtaka mshiriki kukata kuponi na kujaza kisha kuituma MCL makao makuu au ofizi zilizopo kote nchi.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!



7000 symbols left










Banner
Banner




Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.