MPWAPWA KUWA JAGWA BAADA YA MIAKA KUMI.,WATAFITI
NA STEPHEN NOEL MPWAPWA Imeelezwa kuwa baada ya miaka kumi zaidi ya wakazi wapatao wapatao 150,000 laki moja na elfu hamsini wa kazi wa wilaya ya mpwapwa na kogwa wataokosa huduma za maji kabisa kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika vyanzo ya maji vya milima kiboliani na kwa kwamdyanga. Hayo yamebainishwa na watafiti wa huduma za jamii za kituo cha utafiti na mifugo cha Tanzania kilichopo wilayani mpwapwa Mkoa wa dodoma kijulikanacho kama LITI – MPWAPWA. Akiongea na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya mpwapwa amabae kwa sasa amehamia wilaya ya Karagwe Bi Darling Lwegasila mkuu wa chuo cha utafiti cha mpwapwa Dk, Devid Sindalo alisema kuwa kutokana shughuli za kibinadamu zinazo endelea katika vyanzo ya maji vilivyoko kwenye milima kiboliani Wilaya ya mpwapwa wakazi wake watakosa maji ...