WATUMISHI WA HALMASAURI WAISABABISIA HALMASHAURI HASARA YA MIL36

Mpwapwa

BAADHI ya watumishi wa Halmashauri ya Mpwapwa, wameisababishia hasara ya shilingi 36,720,000 kwa mwaka kutokana na kukwepa kulipa ushuru wa vibanda 153 vya biashara wanavyomiliki.
Hasara hiyo ilibainishwa mwishoni mwa wiki kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo ilidaiwa watumishi wanaomiliki vibanda vya biashara wameshindwa kulipa ushuru na hawajachukuliwa hatua za kisheria.
Diwani wa Kata ya Kimagali, Matuluh Kuchela (CCM), alimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri, Alexander Nyaulingo kutoa maelezo ni kwanini baadhi ya watumishi wanaomiliki vibanda hawalipi ushuru ilhali wanajulikana.
Kuchela alisema wakati halmashauri ikiendelea kulalamika kwa kushindwa kukusanya mapato katika maeneo mbalimbali, wapo watumishi ambao wanamiliki vibanda na hawalipi ushuru kwa makusudi.
Alisema inaonesha baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo ambao wamamiliki vibanda wanaisababishia hasara halmashauri ya shilingi 3,060,000 kwa mwezi.
Aidha, alisema kuwa kwa mwaka watumishi hao ambao ni wakaidi katika ulipaji wa ushuru wanaisababishia halmashauri hasara ya sh 36,720,000 kwa mwaka.
Akijibu hoja hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Nyaulingo alisema hakuna sababu yoyote ya mtumishi wa halmashauri anayemikiki kibanda cha biashara kutolipa ushuru.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.