CCM WAHAHA WAWAKUSANYA WANACHAMA KWA MAROLI

• Yakusanya watu kwa maroli mkutanoni

na Chalila Kibuda




VIGOGO na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana walilazimika kutumia jitihada za ziada kuhakikisha mkutano wake unaufunika ule uliofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wiki mbili zilizopita.

Miongoni mwa jitihada hizo, ni kuwapa fursa Waziri wa Ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe, Waziri wa Miundombinu, Dk. John Magufuli, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na wengine kuzungumzia mazuri yaliyofanywa na chama hicho ambayo yanadhihakiwa na wapinzani.

Mwakyembe alitumia mkutano huo kuelezea madudu aliyoyakuta kwenye wizara anayoiongoza, ambayo kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na udhaifu wa serikali ya chama chake ambayo kwa muda mrefu imekuwa na utaratibu wa kulindana, kubebana na kufumbia maovu.

Alisema tayari ameanza kazi kwa kasi na ameomba apewe miezi mitatu kuishughulikia Mamlaka ya Bandari kwani amepata taarifa kuna madudu mengi ambayo yanasababisha serikali kukosa mapato kwa uzembe wa watu wachache.

Waziri huyo alisema matatizo mengine yanatokana na watu kulindana katika kufanya uzembe ambao unagharimu serikali kupata hasara pamoja na kuyafanya mashirika kushindwa kujiendesha yenyewe kwa ufanisi, huku watumishi wakifanya kazi kwa mazoea.

“Bandarini kuna madudu makubwa, suala la bandari kugeuzwa 'supermarket' ya vifaa vya magari ni suala ambalo nitalishughulikia kwa nguvu zote, biashara hii itawang'oa ambao wameota mizizi kama mbuyu kwa kuifanya bandari sehemu ya kufanya madudu, “Nitawafukuza kazi wote ambao wanafanya kazi kwa mazoea wizarani pamoja na taasisi ambazo ziko chini ya wizara yangu.

Katika mkutano huo mawaziri hao walitaabika kukitetea chama na serikali yao kwani walidiriki kutofautiana juu ya upandaji wa nauli kulikosababishwa na kupaa kwa gharama za mafuta.

Wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Steven Wassira akisema ugumu wa maisha, kupanda kwa nauli, bei za bidhaa, na huduma muhimu unaowakabili wananchi ni kwa sababu ya kupanda kwa gharama za mafuta huko Uarabuni, Dk. Mwakyembe amepingana naye kwa kusema wanaopandisha nauli za daladala wana matatizo, na serikali haitowavumilia waendelee na utaratibu huo unaokiuka utaratibu wa kisheria wa kupandisha nauli.

“Juzi nilipanda daladala kutoka Mwenge kwenda Tegeta nikalipishwa sh 500 badala ya sh 400, nikapanda tena daladala hadi Bunju nikalipishwa tena sh 500, nikapanda tena... ukienda Ubungo hadi Kimara hali ni hiyo hiyo, kwa hiyo nikajikuta safari ndogo natumia sh 1500, pesa ambayo kwa Mtanzania wa kawaida hawezi kuimudu kila siku,” alisema Mwakyembe.

Kwa upande wake, Magufuli aliwahakikishia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na suluhisho na kudumu la barabara na kwamba tayari miradi kadhaa inatekelezwa.

“CHADEMA wanasema tu, lakini wao sasa hivi wanafanya maandamano katika lami… nawapongeza sana na ninaamini wataendelea kuandamana katika lami huku wakiendelea kuisema serikali ya CCM vibaya," alisema Dk. Ma

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.