HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA



Na Stephen –noel –mpwapwa.
WANANCHI wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameonyesha wasiwasi wao juu ya vitu vya kihistoria  ya wilaya hiyo vilioachwa na wakoloni iko hatarini kutoweka  kutokana  na  sehemu hizo  za kihistoria kuto kuhifadhiwa   na kulidwa na mamlaka husika.
Wakiongea  na waandishi wa habari  mmoja wa wazee wakongwe wa mji huo  bwana Abinoo Mathiasi   mkazi wa  hazina alisema kuwa  miongoni mwa historia hizo ambazo  ni  njia kuu ya watumwa  iliyokuwa ikotokea  bara  yaani mikoa ya Kigoma  na Tabora  na kuelekea Bagamoyo na Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na Said Majid TippTip na Abushir ambayo kwa sasa iko mbioni kufutika
Mti wa mlumbulumbu ambao kwa sasa umesha anguka na wanachi wameupasua kuni ambapo  palichomwa  kanisa la Anglikana la kwanza  na mfanya biashara ya watumwa  mwarabu Abushir kwa vile watu wa eneo hilo walikuwa wanapinga  biashara  hiyo mwaka 1890 eneo la Vinghawe palipo jegwa kanisa la watakatifu wote.
Aidha alisema  kuwa kisima  walichochokunywa maji  watumwa na bwana  wao katika eneo la  stand Mpwapwa mjini  wakiwa njiani kutoka kigoma  kuelekea Bagamoyo,na  mti uliotumika kuwanyongea watumwa waliokuwa wakishidwa kuendelea na safari  kutokana na ugojwa au uchovu kwa sasa ambao haupotena.
Aliongeza kuwa  sehemu palipojegwa  ofisi za ujenzi za halmashauri ya wilaya ya mpwapwa ambapo palitumika na wajerumani  kama ngome kubwa ya kivita.
Mathias alisema  magofu ya kijiji cha chunyu  ambayo  ilikuwa kama kambi ndogo ya kivita ambayo ilitumiwa na  wajerumani hao kwa sasa yamebaki magofu ambapo alisema siku hadi siku zinavyodhidi kwenda ndo inazidi kuharibika.
Kwa upande  wake  Bi Faith Chali  alisema kuwa  endapo kama  maeneo hayo wangehifadhiwa na kutunzwa  ingekuwa moja wapo ya njia za wilaya hiyo kujiongezea kipato na pia ingekuwa chanzo cha ajira kwa vijana .
Afisa utamaduni msaidizi bi Editha Robert Mbinda alisema “ maeneo hayo yangetunzwa vizuri kama wasemavyo wananchi yangekuwa na manufaa makubwa  kwa halmashauri yetu kwa kuongeza ajira  kwa vijana na  pia  yangetumika kama kituo cha kujifunzia  kwa baadhi ya watu wa historia na kubaki kama kumbukumbu kwa kizazi cha sasa  na cha badae  kama sisi tulivyo yakuta maana yake yalitunzwa”alieleza bi Editha .
Pia  bi Faith alidai viongozi wa halmashauri ya wilaya ya mpwapwa  wajifuunze kwa halamsahuri  za bagamoyo  na Zanzibar  zinazo  tegemea uchumi wao  kwa  watalii ambao huenda kuangalia baadhi ya vitu vya kale  na historia ya utumwa katika Tanzania ambayo inalingana na historia ya  wilaya ya Mpwapwa.
Alitoa lawama kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya  hiyo kwa kumuajili  afisa muhifadhi  mambo ya kale Amani Bendera  na sasa ambae wamembadilishia majukumu na kuwa mwandika vikao vya halmashauri hiyo huku kitengo hicho kikibaki  bila mtu.
Hata hivyo alisema kutokana  na kupungua kwa uwajibikaji na ubunifu  kwa watendaji  wa serikali  kumepelekea  maeneo hayo kuwa hatarini kutoweka na  kutishia historia ya wilaya hiyo kupotea na kuto kuwapo  tena kwa kizazi cha sasa na cha badae.
Afisa Utamaduni  wa halmashauri  ya wilaya  hiyo Reuben Mwatwiza  alisema  kutokana na idara hiyo kuto kuwa na  ruzuku  za mwezi  kumepelekea  baadhi ya maeneo hayo kuyashidwa kuyatunza  na kusababisha  mengine kuanza kutoweka.
Alisema walifanya utambuzi wa maeneo hayo na kuyawekea mipaka  na ambapo   sasa imepita miaka mingi mipaka hiyo baadhi imeharibika na kupoteza  ubora wake  hivyo  kutishia kutoweka kwa historia ya wilaya hiyo.
Amewataka wananchi  na wadau wa maendeleo wilayani hapo kuweza kuunganisha nguvu za pamoja  ili kuweza  kutunza  maeneo ya kiistoria  na rasilimali za kale  katika  wilaya yetu ili iweze kuwa na tija kwa wilaya na wakazi wake.

Comments

  1. ni kweli inasikitisha sana kwani viongozi wanashindwa nini kuyatunza maeneo ya historia kama hayo ushauri nautoa bure waende bagamoyo wakajifunze jinsi ya kuyatunza maeneo muhimu kama hayo by ERNEST JUMA kutoka BEREGE Mbunge mtalajiwa 2020

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.