ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPIGWA NA TEMBOOMANA
Na OMANA GOUTH MPWAPWA Mtu mmoja anayejulikana kwa jina Baraka mlowe (25) mkazi wa kijiji cha pwaga kitogoji cha ikulu wilayani mpwapwa mkoa wa Dodoma amejeruhiwa na tembo na kupasuliwa tumbo hadi utumbo kuwa nje ya tumbo lake. Akizungumza na waandishi wa habari kaka yake majeruhi bwana Geofrey Mlowe alisema kuwa siku ya tukio majeruhi alikuwa na nyumbani na alisikia kuwa tembo wameingia mashambani na wanaharibu mazao na ndipo alipo enda kuangalia hali ya shamba na kuwafukuza wanyama hao, Alisema kuwa ndipo alifika mashambani alikuta tembo hao na alikuta watu wengi wakiwa wana shangaa tembo hao lakini yeye alitaka kuwashangaa kwa karibu ndipo tembo huyo alimrukia na kumwangusha chini na kuanza kumkanyaga na alimchoma na mkonga na ndipo alimtoboa sehemu za tumboni na kumtoa utumbo ukiwa nje. “Alipo kuwa amekamatwa na tembo huyo watu wakapiga kelele na za kuomba msaa...