MAJI KIKWAZO CHA MAENDELEO IDILO WILAYA YA MPWAPWA
New post el-Mpwapwa Wakazi wa kijiji cha Idilo kata ya Mazae wilayani Mpwapwa mkoani hutumia maji yasiyo salama na kutishia kupata magonjwa ya mlipuko hasa kipindi hiki kuelekea msimu huu wa mvua za vuli. Maji hayo yanayopatika umbali km 2 hadi 3 kwa pia ni maji ya makorongoni ambayo ni hatari kwa afya za wakazi hao. Diwani wa kata hiyo bwana Wiliam Vahae amesema wakazi hao hulazimika kuamka alfajili na mapema ili kuwahi maji katika kisima kabla hayajachafuliwa na wanyama wa polini lakini kabla ya wafugaji hawajanza kunywesha Ng,ombe ambao wanakuwa na makundi makubwa ya mifugo. Aidha Vahae amesema kutokana na hali hiyo kumepelekea wakazi wa kijiji hicho kutumia maji ya visima vya asili na makorongo ambayo si safi na salama na kutishia magonjwa ya mlipuko kama kipindupindi. Amesema kufutia tatizo hilo tayari wakazi wa kijiji hicho wamesha changa kiasi cha shilingi million 450,000/=ambazo ...