WAKUU WA MIKOA WAPEWA CHANGAMOTO .JAFFO
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Selemani Jaffo amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha wanaandaa miundombinu ya elimu ya kutosha katika mikoa yao ili wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kupata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza january 2018 wanapata nafasi hiyo. Akizungumza mjini dodoma Waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo amesema kufuatia kuongezeka kwa ufaulu wa asilimia 72.76 kwa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba ofisi yake haina budi kutoa maelekezo hayo ili maandalizi yaweze kufanyika mapema. Kuhusiana na kushuka kwa Somo la kingereza Waziri Jafo anatoa maelekezo. Katika hatia nyingine Waziri Jaffo amewataka makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wahalmashauri zote nchini kuwapokea watumishi 2058 wa sekta ya afya ambao wamepangiwa vituovya kazi kwa kuwapatia stahiki zao. Watumishi waliopangwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 MWISHO. |
Comments
Post a Comment