DC MPWAPWA AWAHADHARISHA WAKULIMA PWAGA.
Mkuu wa wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma bwana Jabiri Shakimweri amewataka wananchi wa vijiji vya Pwaga na Mingui kuto kuuza ardhi kiholela hasa katika kipindi
hiki cha ujio wa serikali mkoani Dodoma
Shakimweri aliyasema hayo juzi alipokuwa akifungua mafunzo
ya kwa wakulima wa vijiji vya pwaga na Mingui wilayani Mpwapwa yaliyofadhiliwa na
Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge (MKURABITA) juu ya kuweza kuitumia ardhi
kama rasilimali muhimu kwa maendeleo ya
mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Aidha Shakimweri amesema kuwa mala baada ya serikali kuanza
kuhamia Dodoma kumeibuka baadhi ya watu
wanao zunguka katika wilaya zote za mkoa Dodoma kununua maeneo ya watu kwa bei nafuu na kuwaacha
wakazi wa maeneo hayo katika hali
ya umaskini na kutishia kuwapo
katika mogohoro ya ardhi.
Mkuu wa wilaya hiyo amesema lazima wanannchi hao kuweza kutumia fursa za hati za kimila za ardhi kwa kuweza kuongeza dhamani ya ardhi kwa kupanda mazao ya biashara ya muda mrefu kama
korosho ambayo imeonekana kufanya
vizuri katika wilaya ya Mpwapwa.
Kwa upande wake Meneja wa urasimishaji ardhi kutoka katika ofisi ya Rais bwana Anton Mushi amesema wamepanga maffunzo hayo kwa wakulima wa pwaga
na Mingui kutokana na vijiji hivyo ni
miongoni wa vijiji vilivyofanyiwiwa Mpango wa matumizi bora
ya ardhi na kupatiwa hati za
kimila .
Mushi amesema
kuwa lengo la mkurabita ni kuweza
kulasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania katika
kijiji cha pwaga ikiwa ni kutenga na kupima maeneo ya kijiji kwa ajili ya
shughuli mbalimbali za kiuchumi na matumizi bora ya ardhi.
Hata hivyo Mushi
alisema kuwa ardhi ni moja wapo ya rasilimali kuu ya na muhimu kama
ikitumika inavyotakikana hasa kwa kilimo kitaweza kubadilisha hali ya kipato cha watanzania na nchini.
Mwenye kiti wa
kijiji cha Pwaga bwana Msemakweli
Chahonza ameongeza kuwa jumla ya mashamaba 1277 yamepimwa na tayari hati 1031 hati
za kimila zimekabithiwa kwa wananchi wa Pwaga ambao wataweza kutumia
hati hizo kama fulsa kama dhamana ya
kuaminika kwa mkulima na kupelekea
kubadilisha maisha ya mkulima
mdogo.
.
Comments
Post a Comment