JAMII YAFICHA TAARIFA ZA UKATILI.
MTANDAO wa polisi wanawake wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma
umesema kasi ya ukatili kwa watoto inasababishwa na jamii kuficha taarifa za
vitendo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa dawati lá njisia katika kituo
cha polisi wilayani hapa Bi Elfrida Mapunda katika maadhimisho ya miaka kumi ya
kuanzishwa kwa dawati hilo.
Bi Mapunda amesema kuwa vitendo vya ukatili vinavyodhidi
kushika kasi vinasababishwa na jamii kuzidi kuvifumbia macho vitendo hivyo au
kamalizana kienyeji bila kufuata sheria na bila kuangalia madhara.
Aidha Bi Mapunda ameitaka jamii kwa kusaidiana na jeshi lá
polisi kuweza kushirikiana katika kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake.
Pia amesema katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa
kwa mtandao huo kumeongezeka kwa taarifa za ukatili ambazo hapo awali zilikuwa
zinafichwa kutolewa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho bi Selina
Chimwaga amesema kuwa kuwa kundi kubwa lá watoto hao wenye mtindio wa ubongo
wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa matibabu kutokana na kuto kuwa na
bima za afya.
Bi Chimwaga amesema watoto wengi wamekuwa wakifungiwa ndani,
wengine kunyeshwa pombe na dawa za usingiz ili kuogopa kuwaambia kwa baadhi ya
wazazi.
Ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2009
kimeweza kuwabaini zaidi ya watoto Zaid ya 5000 wenye matatizo ya utindio wa
ubongo wakiwa wanafungiwa ndani na kukosa haki yao ya Elimu na hivyo wengi wao
wakiwa watu wazima huwa tegemezi.
Mmoja wa walimu anaye fundisha elimu maalun katika shule ya
Msingi Chazugwa bwana Hussein Hussein amesema kuwa watoto wenye ulemavu wa wa
akili hufichwa ndani kutokana na Imani potofu uliopo kwa jamii juu ya watoto
hao.
Bwana Hussein alisema katika shule yake kuna wanafunzi 21
wakiwamo wasichana 8na wavulana 13 japo kuwa wilaya ina watoto wa Namna hiyo
wengi katika wilaya ya Mpwapwa.
Mwisho.
Comments
Post a Comment