MKURUGENZI MPWAPWA AITAKA JAMII KUHAMASIKA KATIKA MAENDELEO.
SHULE ya Msingi Mngangu
wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma inakabiliwa uhaba wa matundu ya vyoo hali hiyo inapelekea kuwapo kwa mazingira magumu kwa walimu na
wanafunzi kwa ya kujifunzia na kusomea.
Mwenyekiti wa
kijiji hicho bwana
Sospiter Nyaombo amesema kufutia hali hiyo bwana jamii
wakajihamasisha na kujenga matundu ya
kumi mbili ya vyoo vitakavyo ondoa adha
kwa wanafunzi kulundikana vyooni
wakati wa mapumziko .
Bwana Nyaombo amesema “mpaka
sasa kupitia nguvu za wananchi tumesha jenga matundu kumi na mbili ya vyoo ambayo yatapunguza adha ya matundu ya
vyoo shuleni hapo lakini kwa kutambua
majukumu yetu tumesha chukua hatua ya kuwaondolea kadhia hiyo watoto wetu ili
wasome katika mazingira rafiki na hatimae kukuza kiwango cha ufaulu shuleni
hapa.”aliongea Bwana Nyaombo.
Aidha mwenyekiti
wa kamti ya shule hiyo bwana Sajilo Nuhu amesema shule hiyo yenye
wanafunzi 461 lakini ina matundundu nane tu ya vyoo yanasababisha mlindikano wa
wanafunzi vyooni lakini pia kutishia kwa
magojwa ya mlipuko hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mvua za vuli.
Bwana Sajilo amesema
pia shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya
madarasa,madawati nasamani zingine za ofisini kwa walimu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa bwana Mohamed Maje
amesema wao kama serikali wameshatoa bati thelathini na mifuko 30 ya sementi kwa ajili ya umaliziaji wa
ujenzi wa vyoo hivyo .
Bwana Maje amewapongeza wanachi wa kijiji cha
Mangangu kwa kuhamasika kuondoa changamoto ya vyoo katika shule yao na
aliwataka wananchi wa vijiji vingine kuweza kuiga mfano wa kijiji hicho katika kutatua changamoto za lkimaendeleo kwa
kutumia nguvu kazi kazi walizonazo na rasilimali zinazo wazunguka.
Comments
Post a Comment