ZAIDI YA BILIONI 15 ZINAHITAJIKA KUKAMILISHA JENGO LA RC DODOMA.
ZAIDI ya Sh.Bilioni 15 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi
wa jengo la Mkuu wa mkoa wa Dodoma ambalo linatarajiwa kuwa ni ofisi ya Rais na
Makamu wa Rais ambapo ujenzi huo kwa sasa umefikia asilimia 56.
Akizungumza wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa
dodoma Dk.Binilith Mahenge wakati wa ukaguzi ujenzi wa jengo hilo Msanifu wa
majengo wa kampuni ya (CRJE) Peter Kibushi amesema fedha hizo sh. bil 15.9 za
awamu ya tano pindi zitakapotolewa zitakamilisha ujenzi huo.
Akisoma taarifa ya ujenzi huo, Msanifu huyo amesema
ujenzi wa jengo hilo ulianza Juni 2009 na utagharimu zaidi ya Sh.Bilioni 25
ambapo hadi sasa fedha zilizotolewa ni takribani Sh.Bilioni 12.
Naye Mhandisi Mshauri wa ujenzi huo, Titus Tesha
amesema wamelazimika kujenga kwa awamu kutokana na mtiririko wa fedha kuwa
mdogo na hivyo kupanga kazi kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Akizungumzia kuhusu utoaji wa fedha kwa ajili ya
jengo hilo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Deogratias Yinza amesema
katika mwaka wa fedha 2017/18 zimetengwa Sh.Bilioni 2.3 kwa ajili ya jengo hilo.
I
Ujenzi huo wa jengo hilo ulianza rasmi june 2009 kwa
kutumia bajeti ya mwaka wa fedha 2009/2010 na ulikadiriwa kugharimu kiasi cha
shilingi billion 15.2 huku ukitakiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu lakini hali
imekuwa tofauti kutokana na mtiririko wa fedha usioridhisha ambao umesababisha
ujenzi huo kuchelewa kukamilika wa muda uliotakiwa.
Comments
Post a Comment