KOROSHO ITAGEUZA UCHUMI WA DODOMA
WAKULIMA
wa Mkoa wa Dodoma wameshauriwa kujikita katika ulimaji wa zao la korosho
kwani zao hilo lina faida kubwa kibiashara tofauti na yalivyo mazao mengine.
Korosho ni moja ya mazao makuu ya
biashara nchini. Kwa sasa zao hili hulimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania,
yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma, Pwani na Tanga.
Takwimu
kutoka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) zinathibitisha umuhimu wa zao hilo kwa
Taifa, ambapo katika msimu wa 2012/13 zao hilo liliiingizia Serikali kiasi cha
Sh bilioni 29.5 kutokana na ushuru wa usafirishaji wa korosho ghafi nje ya
nchi.
Akizungumza
wakati wa ziara yake katika baadhi ya wilaya za mkoa huo Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dr.Binilith Mahenge ameeleza kuwa utafiti umefanywa na kubaini ardhi ya
Dodoma inafaa kwa uzalishaji wa zao hilo.
Akitoa
taarifa ya wilaya kwa Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota
amesema wilaya yake imeanza kuwa na mkakati wa zao la korosho kama zao la
biashara na hadi sasa wameshapokea mbengu ya zao hilo kutoka katika Bodi ya
Korosho.
Aidha
Dr.Mahenge amepingana na wanaodai kuwa Mkoa wa Dodoma ni kame na kusisitiza
kuwa ni lazima wakulima walime mazao yanayo endana na hali ya hewa ya mkoa huu.
Comments
Post a Comment