WAJUMBE WA MKUTANO MKUU UWT WAAONYWA DODOMA.


WAJUMBE wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa  Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Dodoma wameaswa kuchagua viongozi makini na imara watakaokifanya chama kiendelee kuwa imara kutokana na  mkoa huo kuwa makao makuu ya Chama.

Pia amewataka wana CCM kupendana,kupunguza figisu,visasi,majungu,porojo na kuwa ili kufikia maengo ni lazima wanyanyuane na kuinuana kwa lngo la kumfanya kila mmoja atimize yale aliyoyapanga kwa msaada mkubwa wa mwanamke.

Rai hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Dodoma Alhaj Kimbisa wakati akifungua mkutano huo ambapo amesema CCM nyumbani kwake ni Dodoma hivyo viongozi watakaochaguliwa lazima watambue hilo kwa kulinda heshima isipotee.



Aidha amewaasa kutochagua viongozi wenye harufu ya rushwa bali wachague viongozi watakaokuwa wepesi wa kuwaunganisha akina na watakaoifanya jumuiya ijitegemee kiuchumi.



Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe 473  ambapo miongoni mwa nafasi zinazogombewa ni nafasi ya uenyekiti UWT mkoa na wagombea wake ni Elizabeth Kazimila,Neema Majule na Lucy Rutahinurwa.

Nafasi nyingine ni mjumbe wa baraza Kuu mkoa,mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa,uwakilishi kwenda wazazi mkoa,uwakilishi kwenda UVCCM mkoa na wajumbe wa baraza mkoa nafasi mbili kwa kila wilaya.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.