AKINA MAMA WAJIFUNGULIA MAJUMBANI BAHI.
AKINA
mama wajawazito wapata 47 katika kata ya mpalanga Wilaya ya Bahi Mkoani
Dodoma wametajwa kujifungulia nyumbani katika kipindi cha kuanzia mwezi july
hadi septemba mwaka huu jambo linalohatarisha maisha ya mama na mtoto.
Zipo
sababu mbalimbali ambazo zinatajwa kupelekea akina mama wajawazito
kutojifungulia katika zahanati na vituo vya afya ikiwa ni pamoja ni huduma
hiyo kukosekana katika baadhi ya vijiji,miundombinu kutokuwa rafiki na
pengine kupelekea akana mama hao hujifungulia njiani.
akisoma
taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika kikao cha baraza la
madiwani wa halmashsuri hiyo cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18,
diwani wa kata hiyo Daudi Magalamile amesema kuwa sababu hizo zimekuwa ni
changamoto katika maeneo yao.
Diwani
huyo amesema hapo awali kulikuwa na utaratibu wa kuwatoza faini akina ambao
wanajifungulia nyumba ambao utaratibu huo uliwafanya akina mama hao
kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati lakini baada ya kuondolewa
faini hiyo akina mama wengi wamekuwa wakijifungulia nyumba.
Kufuatia
changamoto hiyo diwani huo ameeleza juhudi na hatua za ujenzi wa zahanati
katika kijiji cha chililo zilianzishwa lengo ikiwa ni kutatua tatizo hilo
licha ya kuwa ujenzi wa kituo hicho umekuwa wa kusuasua.
Kutokana
na kusuasua kwa ujenzi huo mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Danford Chisomi akaahidi kuchangia mifuko 10 ya saruji ili kusaidia
ukamilishaji wa zahanati hiyo.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya ibugule Blandina Magawa amemtupia lawama
muuguzi wa zahanati ya kijiji cha ng,ome kwa kushindwa kuwahudumia akina mama
wajawazito na kupelekea kujifungulia nje ya zahanati hivyo kuomba halmashauri
kuwatafutia mganga mwingine.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo serikali na wadau mbalimbali
wa afya wana kila sababu ya kuchukua hatua madhubuti za kuendelea kupunguza
tatizo la akina mama kujifungulia nyumbani au njiani ili kuweze
kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Mwisho.
|
Quick Reply
|
Comments
Post a Comment