MAJI KIKWAZO CHA MAENDELEO IDILO WILAYA YA MPWAPWA
el-Mpwapwa
Wakazi wa kijiji cha Idilo kata ya Mazae wilayani Mpwapwa mkoani
hutumia maji yasiyo salama na kutishia kupata magonjwa ya mlipuko
hasa kipindi hiki kuelekea msimu huu wa mvua za vuli.
Maji hayo yanayopatika umbali km 2 hadi 3 kwa pia ni maji ya
makorongoni ambayo ni hatari kwa afya za wakazi hao.
Diwani wa kata hiyo bwana Wiliam Vahae amesema wakazi hao
hulazimika kuamka alfajili na mapema ili kuwahi maji katika kisima
kabla hayajachafuliwa na wanyama wa polini lakini kabla ya wafugaji
hawajanza kunywesha Ng,ombe ambao wanakuwa na makundi makubwa ya
mifugo.
Aidha Vahae amesema kutokana na hali hiyo kumepelekea wakazi wa
kijiji hicho kutumia maji ya visima vya asili na makorongo ambayo si
safi na salama na kutishia magonjwa ya mlipuko kama kipindupindi.
Amesema kufutia tatizo hilo tayari wakazi wa kijiji hicho wamesha
changa kiasi cha shilingi million 450,000/=ambazo ziko benki kwaajili
ya kusubiri nguvu ya serikali katika mradi huo mkubwa maji kijijini
kwao
Hata hivyo amesema baada Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kuona
jitihada za wanachi hao imetenga kiasi cha shilingi milion 30 katika
kipindi cha fedha mwaka 2017/2018 kwa ajili ya kuchimba kisima kirefu
ambacho kitakuwa suruhu ya uhaba wa maji katika vjiji ya Idilo na
Kisokwe vya kata za Mazae.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Bi Agnes Masinjisa amesema tatizo la
maji katika kijiji hicho limekuwa la muda mrefu na baadhi ya
wanasaiasa waliligeza kuwa mtaji wao wa kisiasa ili kuweza kupata
nafasi za uongozi.
Bi Masinjisa amesema wanapata usumbufu mkubwa kutembea umbali mrefu
kwenda kutafuta huduma hiyo ambapo akina mama na watoto ndio
wamekuwa waathirika wakubwa wa kero hiyo licha kutembea umbali
huo.
Mtendaji wa kata ya Mazae bi Joina Machirika amesema pamoja na
kijiji hicho kuwa na mabomba ya maji yenye vyanzo ya mtiririko lakini
uharibifu wa mazingira umesababisha maji hayo kupungua na kuto kidhi
hitaji la wanachi kijiji hapo.
Comments
Post a Comment