UKATILI WA KINJISIA UWEKEWE MKAKATI MADHUBUTI
SERIKALI ya Mkoa wa Dodoma imewataka wakurugenzi wa
wilaya zote ndani ya mkoa ,sekretarieti ya mkoa pamoja na watendaji wengine
katika ngazi zote kutekeleza kwa vitendo majukumu yote waliyopangiwa kwa mujibu
wa mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Maagizo hayo yametolewa hii leo na kaimu mkuuwa mkoa
wa dodoma ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamoga wakati wa
ufunzguzi wa maadimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili dhidi ya
wananwake na watoto ambapo mbali na hayo pia ametoa magizo kwa maafisa
maendeleo na ustawi wa jamii huku akisistiza kuwa maagizo hayo yatafatiliwa kwa
kadri itakavyotakiwa.
Aidha pia Nyamoga amesema wananchi wengi wamekuwa
wakiwatoa malalamiko watendaji wa vijiji na kata kujihusiha na vitendo
vya rushwa jambo ambalo linadidimiza jitihada za kutokomeza ukatili dhidi ya
wananwake na watoto jambo ambalo kwa mkoa wa dodoma halikubaliki.
Kwa upande wake mwakilishi wa katibu mkuu
wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto idara kuu ya maendeleo
ya jamii,mkurugenzi wa maendeleo ya jamii Patrick Golwike amesema
kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo la ukatili dhidi ya wanawake na watoto
serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imekuwa ikichukua
hatua mbalimbali katika kukomesha tatizo hilo.
Aidha naye mwakilishi kutoka mtandao wa
kutokomeza ukatili wa kijinsia (MKUKI) Sarah Mwaga amekuwa na haya ya kusema.
Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika jijini dar es
salaam na kanda ya kati maadhimisho hayo yanafanyika mjini morogoro ambo kimkoa
yamefanyika Wilaya ya Dodoma.
Comments
Post a Comment