WALIMU WAOMBA KUBORESHEWA MAZINGIRA MPWAPWA

MKUU wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bwana Jabil Shekimweri amewataka waajili kuto kuzalisha madeni Malta kwa wafanya kazi wakati serikali ipo kwenye mkakati mkubwa wa kulipa madeni kwa walimu.
Mkuu wa wilaya huyo aliyasema hayo juzi alipo kuwa akifungua mkutano mkuu wa chama cha walimu wilayani hapo kwa mwaka 2017.

Shakimweri alisema kuwa Tanzania ikiwa inajiandaa kuingia katika uchumi wa viwanda lazima kuwekeza katika Elimu ili kuweza kupata wataalamu watakao hudumu katika viwanda hivyo kwa mstakabali Tanzania mpya.

"Tunapo zungumzia Tanzania ya Viwanda lazima tuwaze juu ya wahudumu katika viwanda hivyo lazima tuwajibike kutoa wanafunzi walio makini watakao fiti katika utaalamu wa viwanda" aliongea Shakimweri.

Aidha Shakimweri ameendelea kuvipigia kelele vitendo vya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya walimu wanaojihusisha na mapenzi na wanafunzi, V walimu kumamatwa na vitendo vya rushwa na uwizi.
Pia Mkuu wa wilaya huyo aliwata walimu hao kujihusisha Pia katika kilimo kuliko kubaki kuzunguka katika tasisi za kifedha ambazo nyingi hazina riba Rafiki na kwa walimu, hivyo alisema kuwa kwa Sasa wilaya ikijipanga kujikita katika kilimo cha korosho walimu wawe mfano kwa jamii inayo wazunguka.

Kwa upande wake katibu wa chama cha walimu wilayani Mpwapwa Bwana Pancras Ngamesha alisema kuwa japo kuwa walimu wanajitahidi kuinua Elimu wilayani Mpwapwa Lakini wanarudishwa nyuma changamoto lukuki zinazo ikabili idara hiyo kama miundo mbinu isiyo kuwa imara ya shule, pamoja uhaba mkubwa sana maji kwa baadhi ya maeneo.

Bwana Ngamesha alisema Mpaka Sasa walimu wanaidai serikali umekuwa ikiidai serikali jumla ya shilingi million 953,703,176.20/=kwa kipindi cha miaka miwili.

Hata hivyo Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Daniel Tito alisema pamoja na Rais kutangaza kuwa Mtumishi yeyote asihamishwe bila kukamilishiwa haki zake Lakin deni la walimu limekuwa likikua kutokana na baadhi ya waajili kuwahamisha walimu pasipo kuwapo na haki zao za msingi.

Hata hivyo Bwana Tito Pia alisema changamoto inayo ikabili wilaya ya Mpwapwa ni kuto kuwapo kwa baraza la wafanya kazi bora walio teuliwa mwaka 2016 na 2017 kuto kulipwa zawadi zao kitu alicho kisema kuwa kinarudisha nyuma ari ya walimu kujituma ndani ya wilaya.

Mwenyekiti wa chama hicho aliwata walimu hao kuweza kutimiza wajibu wao kama ilivyo Kauli Yao ya haki na wajibu, kuliko kubaki kulalamika na baadhi ya walimu kuto timiza wajibu wao.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.