DC WATAKA MGAMBO KUZITUMIA FURSA KUJILETEA MAENDELEO
WANANCHI wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wametakiwa kuzitambua
fursa zinazopatikana katika wilaya hiyo ili kuweza kujiletea maendeleo
kuliko kubaki kulalamika.
Shakimweri aliyasema hayo Jana alipo kuwa akifunga mafunzo ya Mgambo
katika Kata ya Lukole kwa mwaka 2017
Shakimweri alisema kuwa kwa Sasa wilaya ya Mpwapwa ni miongoni zenye
fursa nyingi za kimaendeleo Lakin changamoto inayo wakabili wakazi
wake ni kuto kuzitambua fursa zilizopo au kuendelea kuishi kimazoea na
kubaki kulalamika.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabiri shakimweri akiongea na mgambo hawapo pichani.
Alisema wilaya ya Mpwapwa ni wilaya iliyo zungukwa tasisi nyingi za
kielimu kama tasisi ya utafiti wa mifugo, TARILI, chuo cha Mawakala wa
Mifugo Lita, chuo cha ualimu na chuo cha Maafisa afya na Mazingira
lakini maisha ya wakazi wengi wamekuwa hayaashilii uwepo wa tasisi
hizo.
Hata hivyo mkuu wa wilaya hiyo aliwataka vijana waliohitimu mafunzo ya
Mgambo kuweza kuisaidia wilaya katika kusimamia uharibifu wa mazingira
na kuweza kuishi kiapo walicho kiapa kwa viongozi wa serikali na kuwa
na mahusiano jamii.
Kwa upande wake mshaur wa Mgambo wilaya ya Mpwapwa Stafu sanjet
William Kiwele alisema mafunzo ya Mgambo ni jeshi la akiba ambalo liko
tayari kwa majanga yeyote yanayo weza kutokea ukiwa oparesheni mbali
mbali na kutumika katika shughuli za kimaendeleo.
Pia alisema katika mafunzo hayo jumla ya vijana 420 walianza mafunzo
hayo Lakini ni vijana 180 tu ndio walio bahatika kuhitimu mafunzo
hayo.
Askari mgambo wakifanya mambo yao .hilo zoezi linaitwa kuchoma singe zoezi lililo wavutia wengi.
Mmoja wa Mgambo aliye weza kuhitimu Hayo Clarense Exavery alisema
kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kuwa utimamu wa akili na mwili Lakin
Pia kuzitambua fursa zinazo wazunguka na kuzitumia katika kupata
Comments
Post a Comment