AHUKUMIWA MIAKA 60 JELA KWA KUBAKA WATOTO WA MIAKA 9 NA 12


MAHAKAMA ya hakimu makazi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma imemuhukumu
kifongo cha miaka 60 jela na kupigwa viboko kumi na mbili Bwana Aloyce
Hela (45)
 mkaz wa Mwanakianga baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji.

Kesi hiyo iliyo kuwa inasikilizwa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo
Bwana Pascal Mayumba ambapo ilivuta hisia za wakazi wa Mpwapwa na
watetezi wa haki za watoto wilayani hapa.

Bwana Mayumba ameiiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo
katika tarehe Tofauti kuanzia mwaka 2015 hadi Sasa ambapo alikuwa
akiwabaka watoto wawili wa miaka (9)na miaka (12) wanafunzi wa Darasa
la pili na la kwanza katika moja wapo wa shule wilayani hapa.

Mayumba amesema mtuhumiwa alifanya kosa kinyume na kifungu cha sheria
130na 131 kifungu kidogo cha kwanza cha kanuni ya adhabu iliyo fanyiwa
malejeo mwaka 2002.

Aidha Mayumba ameambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa alifanya
kosa hilo zaidi ya mala mbili na kuwapa watoto hao shilling 200 na
alikuwa anafanya katika chumba kimoja kwa zamu.

Mwendesha mashitaki wa polisi Bwana Godwill Ikema ameiomba mahakama
itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa kutokana na ili kuwa fundisho kwa watu
kama yeye anaendeleza ukatili na unyanyasaji kwa watoto pamoja na
serikali na vyombo vyake vyote kuyapigia kelele matendo yanayo kinzana
na ulinzi wa mtoto.

Akipewa nafasi ya kujiletea mtuhumiwa huyo aliiambia mahakama kuwa
ipunguzie adhabu kwa kuwa ana watoto wawili wanao Soma na wanamtegemea
Pia mama yake ni mzee sana naye anamtegemea.

Mhe Mayumba amesema kutokana na ushahid ulio tolewa na vielelezo
vilivyo tolewa mahakamani bila shaka yeyote hatia imepatikana dhidi
yako na mahakama inakuhukumu kifongo cha miaka 30 jela kwa Hati namba
moja na miaka 30 jela kwa Hati nyingine na viboko 12 ambavyo utapigwa
mbele ya hakimu mkazi mfawidhi .

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.