SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU TAHADHARI ZA MVUA.
SERIKALI
imetoa tahadhari ya mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini
huku ikielekeza wananchi kutumia fursa chanya za mvua hizo kwa shughuli za
maendeleo kama kilimo kwa ajili ya kupanda mazao yanayohitaji maji.
Mbali
na kilimo pia wananchi wametakiwa kutumia mvua hizo kuandaa mabwawa na malambo
kwa ajili ya uvunaji wa maji .
Tahadhari
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera,
Bunge, kazi, ajira,vijana na watu wenye ulemavu Stella Alex wakati akizungumza
na waandishi wa habari.
Amesema
kuwa kamati za usimamizi wa maafa kuanzia ngazi ya kijiji na mtaa zinatakiwa
kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa maafa NO.7 ya
mwaka 2015 na kanuni za usimamizi wa maafa za mwaka 2017.
Amesema
kuwa septemba 4 mwaka huu Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ilitoa utabiri wa
msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Octoba mpaka disemba mwaka huu kwa
maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua na kuonyesha maeneo mengi ya nchi
yanatarajiwa kupata mvua za wastani.
Kwa
sasa tayari baadhi ya maeneo yaliyotabiriwa kupata mvua nyingi yameanza kupata
madhara yalizosababishwa na mafuriko ikiwemo vifo,magonjwa ya
milipuko,uharibifu wa mazao mashambani,uharibifu wa mazingira,mali na
miundombinu ambapo pia inadaiwa madhara yanayoweza kuongezeka kama hatua
stahiki hazitachukuliwa.
Comments
Post a Comment