UMASKINI WA KIPATO CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI-.CDF
EELEZWA kuwa umaskini wa kipato ni mojawapo ya sababu kuu inayo chochea kuwapo kwa mimba za utotoni katika jamii.
Kauli hiyo imebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Jukwaa la Utu wa mtoto (CDF) Bwana Koshuma Mtengeti katika warsha ya siku moja ya kutambulisha mradi na shirika hilo kwa wadau.
Bwana Mtengeti alisema kutokana na utafiti iliyo fanywa na shirika hilo kwa kusaidiana na mashirika mengine walibaini kuwa umaskini wa familia hupelekea familia zenye maisha Mara nyingi Zina pambana kutafuta chakula na mavazi kwa ajili ya watoto wao.
Aidha Mtengeti alisema kuwa alisema kuwa kwa mujibu wa utafiti wa demografia ya Afya Tanzania wa 2016 (TDHS) zilionyesha kwamba asilimia 36%ya wasichana wenye umri wa Kati ya 20-24 waliolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18.
Pia Mkurugenz Mtengeti alisema kuwa Pia utafiti huo ulibaini kuwa asilimia 50%ya ndoa za utotoni inahusisha wanaume ambao ni wakubwa kwa umri wa miaka 5-hadi 14 huoa watoto hao na kusababisha wanawake wengi hawana nguvu za kujadiliana katika Kaya na Mara nyingi hunyanyaswa kingono.
"Tunapozungumzia ndoa za utotoni zinasababisha madhara mengi ikiwamo kuongezeka kwa idadi ya vifo vya kina mama na watoto lakini Pia kuebdelea kuwapo kwa ugonjwa wa fistula kwa akina mama" alieleza.
Kwa upande wake Ofisa Elimu msingi wilayani hapa bi Mery Chakupewa alisema kwa miaka mitatu iliyo pita jumla ya watoto 140 walikatisha masomo kutokana na kupata ujauzito
.
Bi Chakupewa alisema pamoja na kuwapo kwa makatazo, sheria, na taratibu Lakin tatizo la mimba mashuleni limezidi kuongezeka mwaka hadi kitu alicho Sema kinasababishwa na kushuka kwa maadili, umbali wa shule ambazo hutoka watoto hao
Bi Chakupewa alisema pamoja na kuwapo kwa makatazo, sheria, na taratibu Lakin tatizo la mimba mashuleni limezidi kuongezeka mwaka hadi kitu alicho Sema kinasababishwa na kushuka kwa maadili, umbali wa shule ambazo hutoka watoto hao
" hivyo wengi wao hupanga vyumba mitaani na hivyo kukosa uangalizi na kusababisha watoto hao kuwa huru zaidi "alieleza Chakupewa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpwapwa ambae alikuwa mgeni rasmi katika katika warsha hiyo alisema ni lazima wazazi na jamii nzima kurudi katika maadili ili kuweza kuokoa kizazi cha Sasa na cha baadae ili kuwa na taifa lisilo kuwa na wajinga wengi.
Shakimweri alisema kwa baadhi ya watu walio aminiwa katika malezi kama, wazazi, walezi na baadhi ya walimu wamekuwa wakijihusisha kimapenzi na wanafunzi au watoto wanao walea.
Kufuatia Hali hiyo mkuu wa wilaya huyo ameutaka uongozi wote wote wa wilaya na vyombo vyake vinavyo weza kuongeza ulinzi kwa mtoto kwa kufanya kazi kwa ukaribu Zaid ili kuweza kupata takwimu sahihi ili kusaidia wilaya kujua ukubwa wa tatizo lilivyo.
Comments
Post a Comment