MAAFISA MAENDELEO TIMIZENI WAJIBU WENU-WAZIRI WA AFYA.
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii wote kutekeleza wajibu
wao wa msingi kwa kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili
wakiwa shule na nje ya shule.
Taarifa ya utafiti wa hali ya afya ya uzazi ,mtoto
na malaria ya mwaka 2015/2016 inaonyesha kuwa asilimia 27 ya watoto wakike
wanapata mimba wakiwa na umri chini ya umri wa miaka 18..
Tatizo hili lipo zaidi mikoa ya Katavi (asilimia 45),Tabora
(asilimia 43),Dodoma (asilimia 39), Morogoro (asilimia 39) na mkoa wa mara (asilimia
37)
Akizungumza leo mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa
Mkutano mkuu wa 12 wa sekta ya maendeleo ya jamii Waziri Ummy amesema kuwa kupitia
mkutano huo maafisa maendeleo ya jamii amesema kuwa kupitia mkutano huo maafisa
maendeleo ya majii wanatakiwa wanatoka na mikakati madhubuti ya kudhibiti vitendo
vya ukatili katika jamii.
Naye Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba
Nkinga amesema kuwa katika awamu ya sasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii wana
wajibu wa kuelimisha na kuhamsha ari ya wananchi kufanya kazi za uzalishaji.
Kwa upande wake mkurugenzi wa maendeleo ya jamii
tika wizara ya afya maedeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, idara kuu ya
maendeleo ya jamii Patrick Golwike amesema kuwa wao kama maafsa maendeleo ya
jamii wanatakiwa kutambua majukumu yao.
Takwimu za elimu kwenye shule za msingi kwanzia
mwaka 2011 hadi 2015 zinaonyesha kuwa wasichana elfu 39,243 waliacha shule
kutokana na sababu mbalimbali na wasichana elfu 3,806 walikatishwa masomo yao
kwasababu ya mimba.
Kutokana na hayo maafisa maendeleo ya jamii anawataka
kufuatilia mwenendo wa taarifa zitakazotolewa na wakuu wa shule ili kubaini
ukubwa wa tatizo katika halmashauri kwa lengo la kubuni na kupanga mbinu za kukabiliana
na tatizo hilo kwa watoto walio shuleni.
Mwisho.
Comments
Post a Comment